NYOTA WETU
MAPENZI YALIMUUA KANUMBA
—————————————————–
Leo April 7 ni kumbukizi ya miaka 12 ya kifo cha nguli wa tasnia ya filamu Tanzania almaarufu Bongo Movie, marehemu Steven Charles Kanumba a.k.a Kanumba The Great.
Mnamo mwaka 2012 Steven Kanumba alifariki dunia baada ya kusukumwa na kujibamiza ukutani akigombana na mpenzi wake Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye kwa sasa ni mke wa Majjizo.
Akiwa yupo kwenye kilele cha mafanikio na kuitangaza vilivyo nchi kimataifa na kushiriki hadi filamu na wasanii wa Nollywood na kuanza kuchuma matunda ya kipaji chake anaiaga dunia akiwa kijana wa miaka 28 tu.
Uhusiano wake na Lulu ulikua gumzo sababu kuu ikiwa ni umri, Elizabeth Michael alikua bado ni binti mdogo ila mambo mengi hivyo Kanumba akawa anajipigia tu mtoto mwenye umri chini ya miaka 18.
Upinzani wa Kanumba na Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ ulileta mapinduzi makubwa ya soko la filamu, Kanumba akiingiza filamu ya moto sokoni ,Ray nae anaangusha bonge la dude sokoni hapakaliki.
Baadhi ya filamu zake ni The Devil Kingdom,Magic House,Johari,Uncle JJ,Big Daddy,Cross My Sin,Payback,Because Of You,White Maria,The Shock,Moses,Love & Power n.k
Toka afariki tasnia ya filamu Tanzania(Bongo Movie) ni kama imejifia zaidi ya kifo cha mende, imepoteza mvuto kabisa
Hadi leo tukio la kifo chake ni tata, Elizabeth Michael akaja kushtakiwa kwa kesi ya kuu bila kukusudia ambapo mwezi November 2017 akahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.
Akatumikia kwa kipindi kifupi tu na kurudi uraiani kuendelea na raha za dunia.
Endelea kupumzika Kanumba