MICHEZO
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limemteua mwamuzi Beida Dahane aliyechezesha mchezo kati ya Young Africans Sc dhidi ya Mamelodi Sundowns kuchezesha michezo ya soka ya mashindano ya Olimpiki itakayofanyika Ufaransa kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11, mwaka huu.
Dahane (32) ambaye alisimamia mchezo huo ulioishuhudia Yanga ikiondolewa kwenye hatua ya robo fainali kwa penalti 3-2 ni miongoni mwa waamuzi 12 kutoka Afrika ambao wamepata fursa hiyo huku kiujumla wakiteuliwa marefa 89 kutoka nchi tofauti duniani.
Katika mchezo huo uliopigwa Aprili 5, 2024, Dahane alizua gumzo baada ya kukataa bao la kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki ambalo kwa mujibu wa baadhi ya picha za video na za mnato, mpira ulivuka wote mstari wa goli ingawa kwa uamuzi wa refa, haukuvuka wote.
Waamuzi kutoka Afrika walioteuliwa kuchezesha michezo ya Olimpiki mwaka huu ni Karboubi Bouchraw wa Morocco, Mahmood lsmail (Sudan), Diana Chkotesha (Zambia), Fatiha Jermoumi (Morocco), Elvis Noupue (Cameroon), Stephen Yiembe (Kenya), Mahmoud Ashour (Misri), Lahlou Benbraham (Algeria), Ahmed Abdoulrazack (Djibouti), Emiliano Dos Santos (Angola) na Shamirah Nabadda Uganda).
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.