ERIKA DE SOUZA VIEIRA APELEKA MAITI BENKI KUKOPA PESA

0:00

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

HABARI KUU

Polisi nchini Brazil wanamshikilia Érika de Souza Vieira kwa tuhuma za kupeleka maiti ya mjomba wake Paulo Roberto Braga (68) benki , ili achukue mkopo kwa jina lake ambao ni Dola 3,250 za Kimarekani sawa shilingi Milioni nane.

Muda mfupi baada ya Érika kuingia katika moja ya benki huko
Rio de Janeiro akiwa na mwili huo wa mjomba wake alikamatwa na ameshtakiwa kwa kosa la kukiuka sheria inayolinda maiti na kujaribu kuiba na kujipatia pesa kwa njia ya ulaghai.

Picha ya video iliyopandishwa na kituo cha televisheni cha Aljazeera inamuonesha mwanamke huyo akimshikisha kalamu marehemu huyo na kumsihi aweke saini kwenye karatasi ya benki huku pia akiwa ameshikilia kichwa chake.

Maofisa wa benki walishtuka baada ya kuona mwili wa ‘mteja’ huyo ukiwa umepauka sana na ndipo waliposema hayupo sawa.

Polisi nchini Brazil wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kufahamu pia kama kuna watu wengine wanaohusika.

Related Posts 📫

RAINFORD KALABA AFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA...
NYOTA WETU Kiungo mshambuliaji wa TP Mazembe na timu ya...
Read more
Ufahamu Mkoa Wa Singida Nchini Tanzania
Mkoa wa Singida ulianzishwa rasmi Oktoba 15, 1963 ambapo kabla...
Read more
Struggling Bochum snatch 1-1 draw against Leverkusen...
BOCHUM, Germany, 🇩🇪 - Koji Miyoshi scored an 89th minute...
Read more
Liverpool transfer news: Koopmeiners bid launched as...
Arne Slot has taken the patient approach working alongside sporting...
Read more
MAMBA NA KIBOKO WALIOLETWA NA MAFURIKO TISHIO...
HABARI KUU Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wametakiwa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  RAIS WA ROMANIA AWASILI TANZANIA

Leave a Reply