WALIOMUUA MWANAFUNZI WA CHUO HAJIRAT SHABAN WAKAMATWA

0:00

HABARI KUU

Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro kwa tuhuma za mauaji ya Hajirat Shabani (22) mwanafunzi wa chuo cha St. Joseph kilichopo mkoani Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro SCAP. ALex Mkama amesema tukio limetokea tarehe 16 aprili mwaka huu nje ya hosteli za chuo hicho alipokuwa akiishi Hajirat ambapo watuhumiwa hao walimvamia marehemu kwa lengo la kumpora simu wakati marehemu akimzuia kuporwa simu yake ndipo mtuhumuwa mmoja alichomoa kisu na kumchoma sehemu mbalimbali za mwili wake na jambo lililopelekea kupoteza maisha.

RPC Mkama amewataja watuhumiwa hao waliokamwata ni Tyson Eliakim (20) ndiye alimchoma kisu marehemu , mwingine ni Elias Lenjemet (29) alikuwa bodaboda siku ya tukio pamoja Fedrick Nongwa (21) mmiliki wa pikipiki namba MC 285 EDX ambayo ilitumika siku ya tukio.

Kamanda mkama amesema kuwa Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

TIMU ZINAZOWANIA KUMNASA PRINCE DUBE Uongozi wa...
Read more
Serikali yawakumbuka wazee kuja na mpango huu...
HABARI KUU Serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya Jamii Jinsia,...
Read more
DIDDY MAKES ADVANCES TO MAKE ARTIST...
OUR STAR 🌟 U.S. rapper Sean “Diddy” Combs is enmeshed...
Read more
Baker bakes huge cake inspired by Osas...
CELEBRITIES A baker, Ayodele Franca Enyelerue, amazed netizens after she...
Read more
Guardiola demands full commitment from Man City...
Manchester City players have to be completely committed to the...
Read more
See also  IFAHAMU NCHI HII MPYA DUNIANI YA "BHARAT"

Leave a Reply