RS BERKANE YAGOMEA KUINGIZA TIMU UWANJANI MCHEZO WA CAF UKITIWA DOA

0:00

MICHEZO

Mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) kati ya USM Alger ya Algeria na RS Berkane ya Morocco haujafanyika baada ya wageni RS Berkane kuzikataa jezi walizozikuta kwenye Vyumba vya Uwanjani wakidai sio zao.

Awali, RS Berkane walidai jezi zao zilizuiwa Uwanja wa Ndege walipowasili Algeria, wakawaambia hawataruhusiwa kuzitumia kwa kuwa zina Bendera ya Morocco, jambo ambalo lilipingwa na RS Berkane, wakasisitiza wanataka kuzitumia jezi hizo la sivyo hawataingia uwanjani kucheza.

Imeelezwa kuwa Msafara wa RS Berkane ulipofika vyumbani ukakuta jezi ambazo hazina bendera ya Morocco na hivyo wakagoma kuingia uwanjani, baada ya majadiliano marefu wameondoka uwanjani.

Wadau wanasubiri maamuzi kutoka kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa kuwa Kidiplomasia Algeria na Morocco hazina Uhusiano mzuri na hiyo inatajwa kuwa chanzo cha Algeria kukataa uwepo wa Bendera ya Morocco kwenye jezi.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

CHANZO CHA MOTO KARIAKOO CHAANIKWA ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
Read more
Wizkid shares his thoughts as Davido gears...
Davido, the Nigerian music sensation, has just made a thrilling...
Read more
Neymar return overshadowed as Al-Dawsari's hat-trick seals...
HONG KONG, 🇭🇰 - Saudi Arabia's Al-Hilal handed defending champions...
Read more
Praise for Feyenoord after surprise win at...
Feyenoord’s players might not have realised the enormity of their...
Read more
SERIKALI YAJA NA MWAROBAINI KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU...
HABARI KUU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi...
Read more
See also  𝐔𝐓𝐎𝐅𝐀𝐔𝐓𝐈 𝐖𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐍𝐀 𝐅𝐂 𝐀𝐔𝐒𝐁𝐄𝐑𝐆 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 90'

Leave a Reply