YUSUPH MANJI AIBUKA AMTAJA KIGOGO ANAYEFANYA SIMBA KUTOKUFANYA VIZURI

0:00

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

MICHEZO

“Unajua wakati nikiwa Yanga, mtu pekee aliyekuwa ananipa wakati mgumu ni Hans Poppe. Huyu jamaa alikuwa anafanya kazi yake kuonesha kabisa kuwa Dabi inatakiwa kuwa na mvuto, alikuwa akizungumza na watu wanamuelewa, alinipa wakati mgumu sana.

“Hata niliposikia amefariki, ukweli kibinadamu nilisikitika sana kwa kuwa alikuwa ni mtu muhimu kwenye soka, lakini nilijua kabisa kuwa Simba inakwenda kupata wakati mgumu na hiki ndiyo kinatokea leo, nafikiri mechi umeiona na msimamo unaonesha hali halisi ilipo Yanga na Simba kwa sasa,” alisema Manji ambaye alidumu kwenye timu ya Yanga kwa miaka 13 kama mfadhili na Mwenyekiti.

“Tulikuwa tunapambana sana uwanjani, lakini tulikuwa marafiki, alikuwa akizungumza lazima nijue amesema nini, huyu alikuwa ana nguvu kubwa sana kwenye soka la Tanzania na alikuwa anaweza kufanya jambo lolote na watu wakamuelewa.”

“Nafikiri unakumbuka wakati tulipoichapa Simba mabao matatu hadi mapumziko, baadaye wakaja kurudisha yote. Hapa Hans Poppe alihusika, siwezi kukuambia alifanyaje, lakini nguvu yake ilisababisha Simba wakapata sare kwenye huo mchezo, alikuwa na ushawishi wa hali ya juu sana kwa wachezaji.”

Yusuph Manji – Mfadhili na Mwenyekiti wa zamani Young Africans

.

Related Posts 📫

AFTER RAMADAN WE WILL BE ON YOUR...
OUR STAR 🌟 “After Ramadan we will be on your...
Read more
MAHESABU MAKALI YA MANCHESTER UNITED KUTINGA 16...
MICHEZO Kwenye mechi ya jana ya UEFA Champions League, Bruno...
Read more
MWANAMKE AMKOMALIA ASAMOAH GYAN ...
NYOTA WETU. Mahakama imesema Asamoah Gyan (37) amlipe fidia aliyekuwa...
Read more
MAMBO 12 YA KUZINGATIA KABLA YA KUCHUKUA...
MAPENZI Uamuzi wa kuoa na kuolewa unahitaji kutafakari kwa kina...
Read more
MENEJA WA TRA AKAMATWA NA MENO YA...
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia...
Read more
See also  Juve must play at their limits against confident Lille, says Motta

Leave a Reply