Pochettino akerwa na kichapo kutoka kwa Arsenal
MICHEZO
Baada ya kichapo cha mabao 5-0 walichokipokea Chelsea kutoka kwa Arsenal kimemuibua kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino na kusema iwapo kikosi hicho kitaendelea kupokea kichapo basi hawastahili kucheza michuano mikubwa ya Ulaya (Klabu Bingwa & Europa Ligi).
āKuabishwa? Hapana siwezi kulitumia hilo neno kwa wachezaji wetu, sitawalaumu wachezaji, hatuwezi kuwalaumu vijana waliokuja hapa kupambana na timu inayopigania kutwaa taji la Ligi Kuu.
āIkiwa tunataka kuwa katika nafasi tofauti msimu ujao, tunatakiwa kufanya maamuzi ni vigumu kusema tutacheza michuano mikubwa ya Ulaya (UEFA, EUROPA) kwa sasa.
āKama tukishinda Jumamosi dhidi ya Aston Villa ni sawa, tukipoteza tena kama leo (jana) hatustahili kwenda Ulaya.
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.