MAPENZI
1. HAKIKISHA MOYO WAKO UMEMKUBALI. 💯
Yani uwe umempokea moyoni kiasi kwamba moyo❤️ una jua yeye ndiyo mpenzi wa moyo wako💓 na siyo mwingine moyo utoshelezwe na yeye.
2. HAKIKISHA AKILI YAKO IMEMKUBALI.💯
Akili yako iwe inajua yeye ndiye mwenye sifa namba moja za kike au zakiume, na wengine wanafata nyuma yake, ili
usiseme nivile sina jinsi ndiyo nilie mpata nitavumilia tu.
3. HAKIKISHA MWILI WAKO UMEMKUBALI.💯
Nikimanisha tamaa ya mwili wako imkubali, kiasi kwamba shauku ya mwili wako nikuwa na yeye tu muda wote na siyo mwingine.
4. HAKIKISHA MAISHA YAKO YAMEMKUBALI.💯
Yani kipato chako, mipango yako ya maisha imkubali,
ili kuepusha kuwepo na siri na vificho kati yenu.🤔
Watu wengi leo hii kwenye ndoa na mahusiano wanateswa na mambo haya (manne) wako na watu ambao hawajawakubali moyoni.
Japo huenda wamewakubali akilini kutokana na sifa nzuri alizo nazo mwenza wako
Unakuta mwili wako pia haumkubali huyo mwenza wako ndiyo maana migogoro ya kutokuridhishana kwenye mahusiano nimingi sana,
Unakuta mwiliwako unahisi ana mapungufu na una mtamani mwingine, inapelekea kuwa chanzo cha usariti
Unakuta mwingine kipato chake anakificha kwa sababu anajua mwenza wake niadui wakipato chake akijua tu atatumia vibaya. Hali hii inapelekea uaminifu kuvunjika ndani ya ndoa au mahusiano.