MICHEZO
Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally ameibuka na kuandika ujumbe kumuhusu Mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast Fred Michael ‘Funga Funga’.
Mshambuliaji huyo alifunga moja ya mabao mawili yaliyoipa ushindi Simba SC katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Muungano 2024 dhidi ya KVZ uliopigwa jana Jumatano (Aprili 24), Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
Ujumbe wa Ahmed Ally umenza na Kichwa cha habari – TOP SCORERS WA MUUNGANO ISRAH & FREDDY FUNGAFUNGA.
“Wakati mwingine Matokeo yasiyoridhisha ya timu huwa yanafifisha ubora wa mchezaji mmoja mmoja au matokeo mazuri ya timu hua yanaficha madhaifu ya mchezaji mmoja mmoja.
Fredy Michael Fungafunga tangu amewasili Simba Sports amefunga jumla ya Magoli 10 katika mashindano yote aliyoshiriki ni wastani mzuri sana kwa mshambuliaji.
Champions league 1
Ligi kuu ya NBC 4
Kombe la Crdb 4
Kombe la Muungano 1
Imani yangu ni kwamba kadri anavyopata muda wa kucheza, kadri anavyoaminiwa ndivyo anathibitisha ubora wake.
Kwetu sisi Wana Simba jukumu letu ni kumuunga mkono Mshambuliaji wetu na tukumbuke ya kwamba hii ndio nafasi ngumu zaidi kwenye mpira duniani kote.
Kwa alichokionesha Fredy hatuna budi kusamama nae ili atufikishe kwenye kilele cha mafanikio”