MICHEZO
Wachezaji wa Chelsea bado wanamuunga mkono Kocha wao mkuu, Mauricio Pochettino licha ya matatizo yao msimu huu, kwa mujibu wa ripoti.
‘The Blues’ wanaweza kumaliza msimu wakiwa nje ya katika nafasi ya kufuzu Ligi ya Europa mwaka wa pili mfululizo, baada ya kudhalilishwa kwa mabao 5-0 na wapinzani wao Arsenal, huku Jumamosi wakitoka sare ya 2-2 na Aston Villa.
Shinikizo linaongezeka kwa Pochettino, kocha huyo mwenye umri wa miaka 52, bado anaheshimiwa sana katika chumba cha kubadilishia nguo, huku Standard ikiripoti kuwa wachezaji wanamuunga mkono.
Nahodha Reece James na msaidizi wake, Ben Chilwell, wameshindwa kutoa ushawishi na usaidizi mkubwa kwa kocha Pochettino kama walivyotarajia, kutokana na majeraha.
Baadhi ya wajumbe wa bodi wanaamini Pochettino anastahili kuendelea na nafasi yake kuelekea msimu ujao, kwani wanatambua changamoto alizokabiliana nazo na kupongeza juhudi zake za kuvuka mazingira magumu.
Muargentina huyo alisaini mkataba wa miaka miwili na Chelsea msimu uliopita wa majira ya joto ambao ulijumuisha chaguo la miezi 12 zaidi.
Na kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu huu, Pochettino atakuwa akitumia kila juhudi kudumisha nafasi yake katika kiti cha moto huko London Magharibi.
Anabakia na imani kwamba mbinu zake hatimaye zitaleta majibu kama ilivyokuwa wakati akiwa na kikosi cha vijana cha Tottenham Hotspur.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.