VYAMA 11 VYA LAANI KAULI YA TUNDU LISSU

0:00

HABARI KUU

KUFUATIA Kauli za hivi karibuni za Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA -Tundu Lisu, Vyama 11 vya Siasa Zanzibar vimelaani vikali kauli hizo ambazo wanadai kuwa ni kauli za Kebehi na uchochezi zinazolenga kuleta ubaguzi kwa Watanzania kupitia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akitoa wasilisho la Pamoja la Viongozi wa Vyama 11 vya Siasa juu ya kauli hizo, Mwenyekiti wa Chama cha ADA TADEA Juma Ali Khatib amesema kauli zilizotolewa na Tundu Lissu ni kauli za kibaguzi ambapo wameziomba Mamlaka husika ikiwemo Msajili wa vyama vya siasa pamoja na vyombo vyengine kuangalia kwa makini hatua za kuchukua kwa kiongozi huyo na chama chake.

“Sisi Vyama 11 vya siasa hatuungi mkono kauli zako Tundu Lisu na tunazilaani, matamshi yako ya kibaguzi kwa kuonesha wazi wazi watu wa upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawana haki ya kufanya kazi upande mwingine na huu ni ubaguzi, uchochezi na kuonesha wazi wazi umefilisika kimawazo, kifikra na kisiasa na kutafuta Kiki za kisiasa,”amesema.

“Kwa msingi huu alioonesha Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA ni dhahiri anawaambia wananchi kwamba yeye ni mbinafsi, mwenye uchu wa madaraka, mchonganishi, mfitinishaji na mwenye dhamira ovu kwa Muungano wetu,” ameongeza.

“Tunavitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini, pamoja na msajili wa vyama vya siasa kufanya uchunguzi wa kina juu kauli anazozitoa ndugu Tundu Lissu kupitia kwenye majukwaa ya kisiasa kama ni za kwake au anatumwa na chama chake na ikithibitika Msajili wa vyama kisiasa achukuwe hatua kwa mujibu wa sheria kutokana kuwa kauli hizo zinalengo la kuligawa taifa letu,” ameeleza

Vyama vilivyotoa tamko hilo ni ADA TADEA, CCK, NLD, Demokrasia Makini, NCCR- MAGEUZI, TLP, UPDP, SAU, UMD, NRA na Chama cha DP.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MUME WA RIHANNA AFUNGUKA JUU YA MKE...
NYOTA WETU. ASAP ROCKY hakuacha tabasamu lake lififie alipokuwa akijadili...
Read more
Real goalkeeper Courtois suffers abductor injury
Real Madrid goalkeeper Thibaut Courtois has been diagnosed with an...
Read more
Madhara Ya Kope za Bandia
Kope za mtu za asili hufanya kazi muhimu, hulinda macho...
Read more
Naomi osaka will escape Billie Jean King...
Japan's Naomi Osaka said she will skip next month's Billie...
Read more
MENEJA WA TRA AKAMATWA NA MENO YA...
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply