HABARI KUU
Aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema ameeleza kuwa hakuna vita ya nafasi ya kugombea Urais ndani ya Chama hicho katika uchaguzi ujao huku akisema amewahi kumsikia Makamu mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu akiweka wazi kuwa hawezi kuchukua fomu ambayo imeguswa na mwenyekiti wake Freeman Mbowe
Kumekuwa na mijadala mitandaoni ikieleza kuwa kuna mvutano wa nani agombee nafasi ya urais ndani ya chama hicho
“Nimeona andiko la BOB Wangwe na maandiko mengine ya watu wengi pamoja na ushauri wake.Jibu langu kwenu ni hili, tukiwa Arusha mahali fulani kwenye mazungumzo yetu ambapo nilikuwepo pamoja na Kamanda Wenje, Heche,Msigwa na Mkti F.Mbowe, Mh Lissu aliongea maneno haya “
“ Nanukuu “ Kaka , Mwenyekiti , ulibeba chupa ya damu nisife wkt nimeshambuliwa kutoka Dodoma ukiwa umesimama kwenye ndege mpaka Nairobi,na ulikaa Nairobi na wenzako hawa muda wote wa matibabu yangu , siwezi kuchukua fomu utakayogusa kwenye Chama hiki,tusiruhusu wapambe watuharibie CHAMA “
“Maneno haya niliyasikia Mimi, Heche, Msigwa, Wenje na Mwenyekiti Mbowe.Hakuna vita kwenye nafasi ya Urais CHADEMA isipokuwa kuna wapambe wajinga na CCM haswa ktk muelekeo wa siasa 2024/2025” ameandika Lema kwenye mitandao ya kijamii .