JELA MIAKA 30 KWA KUMMWAGIA TINDIKALI USONI MCHUMBA WAKE

0:00

HABARI KUU

Mohamed Mwarandu Kombe (30), amehukumiwa miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kummwagia tindikali usoni aliyekuwa mchumba wake, Fatma Kaingu (23).

Hukumu hiyo, imetolewa na Mahakama ya Mombasa Nchini Kenya baada ya mshitakiwa kupatikana kosa hilo lililomsababishia Fatma kuwa kipofu.

Hakimu mkaazi Mwandamizi, Gladys Olimo amesema amezingatia ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, na ule wa mlalamikaji ulioambatana na ripoti za matibabu.

Katika ushahidi wa kitabibu, Madaktari walisema macho yake yaliharibika zaidi na hivyo kupoteza uwezo wa kuona na kwamba haingewezekana kumtibia kutokana na jinsi yalivyoathiriwa na kemikali hiyo.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

ANNIE IDIBIA GUSHES OVER HER MAN
CELEBRITIES Taking to her Instagram page to share a photo...
Read more
Southampton must sack Russell Martin immediately
Southampton’s players should be angry that they threw away two...
Read more
13 WAYS ON HOW TO SETTLE DISAGREEMENTS...
LOVE ❤ 1. Pray for calmness and unity in your...
Read more
Barcelona have cooled their efforts to sign...
Kimmich had emerged as a leading target for Barcelona earlier...
Read more
JURGEN KLOPP AIONYA MANCHESTER UNITED DHIDI YA...
MICHEZO Kocha Mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp ameionya Manchester United...
Read more
See also  MPANGO: AOMBA WENYE URAIA WA TANZANIA KUPEWA KAZI SGR

Leave a Reply