Kylian Mbappe amethibitisha kuondoka PSG baada ya miaka 7

0:00

MICHEZO

Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappé amethibitisha kuwa ataondoka klabuni hapo mwisho wa msimu huu. Mbappé amesema hayo kupitia picha mjongeo kwenye mitandao ya kijamii ingawa hajabainisha ni wapi ataelekea.

Paris Saint-Germain hawajamjumuisha Kylian Mbappe kwenye chapisho la mtandao wa kijamii wakitangaza jezi zao mpya hali inayoashiria kuwa nyota huyo raia wa Ufaransa hayupo kwenye mipango yao ya msimu ujao.

Inaaminika kuwa mfungaji huyo wa muda wote wa PSG tayari amefikia makubaliano ya kujiunga na vigogo wa Uhispania, Real Madrid ingawa hakuna klabu iliyoweka bayana ukweli huo.

Baadhi ya wachezaji wa PSG wameonekana kwenye chapisho la klabu hiyo kwenye mitandao ya kijamii wakiwa na jezi hizo mpya, wakiwemo Marquinhos, Nuno Mendes na Lucas Hernandez lakini Mbappe hakuonekana.


Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WHY MEN DELAY GETTING MARRIED
❤ 1) FEAR (MARRIAGE PHOBIA) Many bachelors actually fear Marriage...
Read more
HISTORIA YA MADILU SYSTEM
Amezaliwa:28 Mei 1952 Amekufa:11 Agosti 2007 Jean de Dieu Makiese kama...
Read more
CHIOMA ADELEKE REVEALS HOW SHE MET DAVIDO
OUR STAR 🌟 Chioma Adeleke, also known as Chioma Avril...
Read more
Uke Wenye Afya bora hauna Harufu wala...
🍂Utunzaji wa uke ni jambo la muhimu sana kwa mwanamke....
Read more
Mamelodi yampa thank you kocha Rhulani Mokwena
Mamelodi Sundowns na Kocha Mkuu, Rhulani Mokwena wamefikia makubaliano ya...
Read more
See also  NEWCASTLE KUMRUDISHA DAVID DE GEA

Leave a Reply