RAILA ODINGA ATAJA VIPAUMBELE AKICHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA AU

0:00

HABARI KUU

Kiongozi wa Azimio, Raila Odinga ameeleza majukumu ambayo atatekeleza iwapo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).

Mambo hayo ni pamoja na kuhakikisha AU inafadhili programu na shughuli zake yenyewe.

Odinga pia anaona Afrika inaweza kufanya vizuri zaidi katika kilimo na ndipo anasema atahimiza utoaji wa pembejeo za kilimo zenye ubora wa hali ya juu ili kuongeza uzalishaji maradufu.

Hatua hiyo anasema itaihakikishia Afrika chakula cha kutosha na kukuza biashara ya bidhaa na huduma za kilimo barani Afrika sambamba na kukuza miradi ya kuongeza mnyororo wa thamani ili kuhamasisha na kuongeza thamani ya mauzo ya nje ya ya mazao ya kilimo.

Jambo lingine katika mipango yake akikwaa nafasi hiyo ni kuondoa tatizo la Waafrika wanapotaka kufika katika baadhi ya nchi barani Afrika kulazimika kwenda hadi Ulaya na kisha kurudi maeneo hayo ya Afrika.

“Inasikitisha kwamba miaka 60 ya uhuru, bado kuna maeneo Waafrika wanapaswa kusafiri kwa ndege hadi Ulaya ili kuungana na sehemu fulani za Afrika na kuhitaji pesa nyingi na visa. Hatuwezi kuendelea na hali hiyo.

“Zaidi ya hayo, ni matumaini yangu kuwa nikiwa mwenyekiti wa AUC, nitalisaidia Bara la Afrika kutekeleza ndoto zilizoahirishwa kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kufanya Mto Nile kupitika wote na kuunganisha Bahari ya Atlantiki na Ziwa Victoria hadi Ziwa Tanganyika ili kuongeza ufanisi katika usafiri wa majini,” Raila anasema.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WATOTO NANE WAFA KWA KULA NYAMA YA...
HABARI KUU Watoto nane na Mwanamke mmoja wamefariki dunia baada...
Read more
WANAOREKODI WANAWAKE UTUPU WANASWA DAR
MAGAZETI
See also  MKUU WA WILAYA ATOA AMRI YA KUWACHAPA VIBOKO WANAOTAKA KUVUNJA MUUNGANO
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
MANCHESTER CITY NA BERNARDO SILVA NDOA YAO...
MICHEZO Mshambualiji kutoka nchini Ureno na Klabu Bingwa nchini England...
Read more
NDOTO YA KOCHA SVEN-GORAN ERIKSSON YATIMIA AKIWA...
NYOTA WETU Meneja wa zamani wa timu ya Taifa ya...
Read more
FAIDA ZA TANZANIA KUWA NCHI YA AMANI...
HABARI KUU Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply