Burundi yaishutumu Rwanda kuhusika na shambulio la Bujumbura

0:00

HABARI KUU

Burundi imeishutumu Rwanda kuhusika katika shambulio la guruneti ambalo liliwajeruhi watu 38 karibu na Soko Kuu la zamani mjini Bujumbura.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama Pierre Nkurikiye amefahamisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakipata mafunzo nchini Rwanda kupitia kundi la waasi la Red Tabara ambalo limekuwa liishambulia Burundi.

Amesema kuwa watu sita wamekamatwa Kwa shutuma za kuhusika na shambulio hilo,uchunguzi ukiwa unaendelea kufanyika ili kuwabaini watu wengine.

Hilo linakuwa shambulio la pili baada ya lililotokea maeneo ya Kamenge wiki moja iliyopita na kujeruhi watu sita, mmoja akipoteza maisha baada ya kufikishwa hospitalini.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  CHARLES KITWANGA awatetea polisi kuhusu rushwa na kuwabambikia raia kesi
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading