BULAYA AIKUMBUSHA SERIKALI KULIPA DENI LA BILIONI 18

0:00

HABARI KUU

Mbunge wa Viti maalumu, Ester Bulaya ameikumbusha Serikali kulipa madeni ya Vyombo vya Habari ili viwezi kujiendesha, kauli ambayo inakuja ikiwa wiki moja imepita tangu Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko kuhimiza suala hilo.

Akiongea hii leo Mei 16, 2024 Bungeni Jijini Dodoma Bulaya amesema Serikali inadaiwa zaidi ya bilioni 18 na Vyombo mbalimbali vya Habari ambavyo vinategemea matangazo kutoka serikalini, huku akimuhoji Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kuhusu suala hilo.

Amesema, “wanapolipwa ndio wataanza kulipa mishahara, wataweza kujiendesha na hapo kuna baadhi ya vyombo vingine havijaorodheshwa katika madeni hayo, vyombo vingine binafsi zaidi ya bilioni saba ziko nje hawa watu watafanyaje kazi? Mhe. Nape sasa unadhani kwa madeni sugu hayo unadhani watajiendeshaje.”

Bulaya ameongeza kuwa, “Sisi waandishi wa habari kazi yetu kufanya kazi tu hatuna wa kututetea mpaka ifike leo humu ndani tuanze kuzungumza hii sio Sawa tunaomba hawa watu walipwe, mbona kuna taaluma nyingine hawakopwi, kuna taswira hapa imejengeka kama Wanahabari ni kama watu wamefeli sehemu fulani wamekuja kutafuta ajira, hii siyo.”

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WATU 7 WAKAMATWA KWA KUGOMEA CHANJO
HABARI KUU Watu saba wote Wakazi wa Kijiji cha Kalambo...
Read more
The Inspector-General of Police, Kayode Egbetokun, has...
The Police Chief made the clarification while speaking at a...
Read more
MUME WA RIHANNA AFUNGUKA JUU YA MKE...
NYOTA WETU. ASAP ROCKY hakuacha tabasamu lake lififie alipokuwa akijadili...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA HIVI LEO 25/06/2024
MAGAZETI
See also  Tafakari ya Askofu BAGONZA Juu ya Uteuzi na Utenguzi wa Rais SAMIA SULUHU
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
TANZANIA YAIBABUA NIGER
MICHEZO Tanzania imeanza vyema kampeini za kufuzu fainali za kombe...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply