0:00
NYOTA WETU
Matokeo ya uchunguzi wa mwili wa marehemu mwimbaji, Ilerioluwa Aloba, almaarufu Mohbad yametoka.
Kwa mujibu wa ripoti inadai kuwa wataalamu wameshindwa kubaini sababu ya kifo cha mwanamuziki huyo kwasababu mwili uliofanyiwa uchunguzi ulikuwa umeharibika sana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana May 15,2024 Wakili Mkuu wa Serikali nchini Nigeria Wahab Shittu amesema kuwa “uchunguzi uliofanywa na madaktari unadai kuwa wameshindwa kujua sababu ya kifo cha mwanamuziki huyo kwani wakati vipimo vinafanyika mwili wake ulikuwa umeharibika sana’.
Mohbad alifariki dunia September 12,2023 kifo chake kilikuwa na utata ambao ulipelekea mwanamuziki Naira Marley kukamatwa kwa kutuhumiwa kuhusika na kifo hicho.
Related Posts 📫
HABARI KUU
VLADIMIR Putin amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa Rais...
Wanaochelewesha mshambuliaji Jean Baleke (23) kutangazwa na Young Africans ni...
MICHEZO
Kikosi cha Simba SC kimewasili salama mjini Cairo, Misri...
MICHEZO
Vinara wa Bundesliga, Bayer Leverkusen wanakaribia kupata taji lao...
In a significant move ahead of the upcoming 2025 Africa...