Serikali kuja na mpango huu wa usimamizi wa fedha za mikopo

0:00

HABARI KUU

Serikali ipo katika maandalizi ya usimami wa mikopo ya asilimia 10 kwa kuamua kuanzisha kitengo maalumu cha usimamizi wa Mikopo hiyo kwa ngazi ya Wizara, na kamati ya usimamizi wa mikopo katikati ngazi ya Mikoa, Halmashauri na Kata.

Ameyasema hayo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Zainabu Katimba Bungeni Jijini Dodoma hii leo Mei 17, 2024 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Christina Christipher Mnzava.

Mnzava alitaka kujua je, Serikali imejipanga vipi katika usimamizi wa mikopo ya asilimia 10, pindi itakapoanza kutolewa tena kuanzia Julai mosi?

Akijibu swahi hilo, Katimba amesema, “timu iliundwa kufanya mapitio na kuhakikisha unatengenezwa utaratibu bora zaidi kwa ajili ya kuhakikisha Mikopo, hii inatoka na inaenda kuwanufaisha walengwa na tayari katika Muundo wa usimamizi wa mikopo hii.

Amesema”kutaanzishwa Kitengo cha usimamizi wa Mikopo katika ngazi ya Wizara Ofisi ya Rais TAMISEMI na kamati za usimamzizi wa Mikopo katika ngazi ya Mikoa, Halmashauri na Kata, mikopo hii inayotokana na Mapato ya ndani ya Halmashuri, ilisitishwa kutokana na maelekezo ya Serikali ya kuangalia upya utaratibu na changamoto zilizokuwepo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

POLISI ARUSHA YAWAKAMATA WAHALIFU WA DAWA ZA...
HABARI KUU Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema hali ya...
Read more
Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo...
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumamosi Juni 01, 2024 na...
Read more
CLEMENT MZIZE NA PRINCE DUBE WAZIKUTANISHA KATI...
MICHEZO Wakati tetesi zikieleza kuwa Uongozi wa Azam FC umewasilisha...
Read more
KISSINGER AAGA DUNIA ...
NYOTA WETU
See also  KINZUMBI YANGA MUSONDA MAZEMBE
Mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani ambaye aliwahi pia...
Read more
Lafey MP Launches Dam and Borehole Projects...
Lafey Member of Parliament (MP) Mohamed Abdikheir has taken a...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply