NYOTA WETU
Mwanamuziki mashuhuri wa Marekani, Sean “Diddy” Combs amezungumzia juu ya video ya mwaka 2016 iliyovuja hivi karibuni ikimwonesha akimshambulia kwa kumkamata, kumsukuma, kumsukasuka, kumburuza na kumpiga mateke mpenzi wake wa zamani, Cassie Ventura.
Kutokana na video hiyo Diddy ameomba radhi juu ya kitendo alichoonekana akikifanya na kukubali kuwajibika kwa aliyoyafanya huku akiahidi kuwa mtu mwema na akijutia kwa kile aliyoyafanya.
“Tabia niliyoionesha kwenye video hiyo siwezi kuitetea. Ninawajibika kikamilifu kwa vitendo vyangu kwenye video hiyo,”
amesema Diddy kwenye taarifa yake ya video iliyochapishwa kwenye Instagram.
Video ya shambulio lake iliibuka katikati ya kesi ya hivi majuzi ya aliyofungua Cassie dhidi yake Diddy, ambapo amemshutumu kwa kumfanyia unyanyasaji kwa miaka mingi.