SABABU 10 ZA MIMBA KUHARIBIKA

0:00

AFYA

” HIZI HAPA SABABU KUMI MUHIMU ZA MIMBA KUHARIBIKA – ( MISCARRIAGE ).

Kati ya mimba 100 zinazobebwa ni 80 tu ndio zinafika kuzaliwa, yaani asilimia ishirini ya mimba zinazobebwa huharibika hata kabla ya kufika miezi mitatu.

Kuna sababu nyingi zinazoweza sababisha mimba kuharibika lakini leo nitaeanda Kuongelea zile muhimu ili kila mtu kama iko ndani ya uwezo wake aweze kuzuia Kuharibika pale anapopata mimba au Kumsaidia Jamaa Yake wa Karibu au Mke Ili Kuepuka na Kupunguza Kiwango Cha Tatizo hili.

” Hizi Zifuatazo ndiyo Sababu Zinazosahabisha mimba Kuharibika.

  1. Matatizo ya vimelea vya urithi: kawaida mbegu za mwanaume huchangia pea 23 za vimelea vya urithi yaani chromosomes na yai la kike huchangia vimelea 23 pia kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa, lakini kwenye hali isiyo ya kawaida namba hiyo ikiongezeka au kushuka husababisha mimba kutoka ndani ya muda mfupi.
  2. Magonjwa; kuna magonjwa mengi endapo hayatatibiwa kwa muda muafaka husababisha mimba kuharibika muda wowote ule yaani inaweza kua mwanzoni au mwishoni.mfano. malaria, kisukari, pressure, kaswende, virusi vya ukimwi, U.T.I, toxplasmosis,rubella, na herpes simplex virus.
  3. Matatizo ya kizazi; kuna magonjwa mengi yanayoathiri kizazi moja kwa moja na huweza kuleta kutoa mimba kirahisi sana mfano wa magonjwa hayo ni uvimbe wa ndani ya kizazi,ulegevu wa mlango wa uzazi na kadhalika.
  4. Matumizi ya dawa; ukiwa mjamzito hutakiwi kutumia dawa yoyote bila kuandikiwa na daktari, kuna dawa nyingi sana zinaweza kuharibu mimba mfano fragile, albendazole,misoprostol, dawa ya mseto ya malaria, doxycline, na nyingine nyingi.
  5. Utapiamlo; mwanamke mwenye upungufu wa madini muhimu mwilini kama calcium, potassium na sodium lakini pia wanga, protini, vitamini na kadhalika. upungufu huu humfanya mwanamke ashindwe kubebeba mimba mpaka kujifungua na hata akijifungua huweza kuzaa mtoto mwenye mapungufu fulani ya kiakili.
  6. Matatizo ya homoni; mwanamke ana kiwango maalumu cha homoni za uzazi ambacho anatakiwa awe nacho ili mimba iweze kutungwa na kukua. kiwango hiki kikiwa juu sana au chini sana husababisha mimba kuharibika.
  7. Aina ya maisha ya mjamzito; matumizi ya pombe na sigara kipindi cha ujauzito ni hatari sana kwani huingilia mfumo wa homoni na uzazi na kusababisha mimba kuharibika.
  8. Umri mkubwa; kubebe mimba kwenye umri mkubwa huchangia sana mimba kuharibika kwani kipindi hiki viungo vya uzazi na mfumo wa homoni unakua umepungua nguvu sana hivyo mimba za ukubwani sana hasa zaidi ya miaka 35 hutoka kirahisi kuliko mimba za vijana wadogo.
  9. Mazingira ya kuishi; maeneo mengi karibu na viwanda au huduma za mionzi ya hospitali hua kuna mionzi hatari ambayo huweza kuingia kwa mama na kuharibu mtoto aliyeko tumboni lakini pia uwezo wa kuzaa huko mbele ya safari.
  10. Upungufu wa damu; kipindi cha ujauzito akina mama wengi hua na damu chini ya kiwango kutokana na mabadiliko ya kimaumbile, lakini upungufu huo ukizidi zaidi husababisha uchungu kuanza kabla muda na mimba kuharibika.
See also  MVUA YAFUKUA MAKABURI ,MIILI YASOMBWA

Mwisho; kila mtu anahitaji mtoto katika kipindi fulani cha maisha yake hivyo ni vizuri kujilinda na vyanzo hivyo kabla na baada ya kupata ujauzito kwa kufuata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa afya na kukaa mbali na mazingira hatarishi ya kuharibu ujauzito.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Mawakili wapata pigo mmoja afariki akihudhuria mkutano...
Wanachama wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), wameuaga mwili wa...
Read more
AFA BAADA YA KUWAPA WANAE SUMU
HABARI KUU Mkazi wa Kijiji cha Mashese, Daines Paul Mwashambo...
Read more
Republican candidate, ex-US President, Donald Trump, has...
Trump announced this in a one-sentence post on his Truth...
Read more
Video of Wizkid and his partner Jada...
The couple made heads turn as they attended the event,...
Read more
ROBERTINHO AIKAANGA SIMBA ...
MICHEZO Aliyekuwa kocha mkuu wa Simba SC. Robertinho amekosoa usajili...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply