Iran kufanya uchaguzi mkuu kumpata mrithi wa Ebrahim Raisi

0:00

HABARI KUU

Baada ya kifo cha Rais wa Iran Ebrahim Raisi nchi hiyo imetangaza kuwa itafanya Uchaguzi wa Urais Juni 28.

Iran itafanya uchaguzi huo kutokana na kifo cha Ajali ya Helkopta ya Rais huyo pamoja na baadhi ya Maofisa wa Serikali ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Serikali IRNA, tangazo la tarehe ya uchaguzi wa 14 wa rais nchini humo limekuja baada ya mkutano kati ya wakuu wa Mahakama, mamlaka ya utendaji na sheria.

Usaili wa wagombea utaanza Mei 30, ripoti hiyo ilisema, ikiongeza kuwa kampeni zitafanyika Juni 12 hadi 27.

Raisi Ebhahim alikuwa akirejea kutoka kwa sherehe za uzinduzi wa bwawa kwenye mpaka wa Iran na Azerbaijan Jumapili wakati ajali hiyo ilipotokea, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Serikali ya Iran.

Ajali hiyo pia ilisababisha vifo vya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian, na vile vile vya Malik Rahmeti, Gavana wa jimbo la Azerbaijan Mashariki, na Imam Ayatollah Ali Hashim wa mkoa wa Tabriz.

Mohammad Mokhber, Makamu wa kwanza wa rais wa Iran, aliteuliwa kuwa Kaimu Rais Jumatatu baada ya kifo cha Raisi.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

England's Carsley stays mum on job aspirations...
HELSINKI, - Lee Carsley was thrilled to see England back...
Read more
Dangers That Damage Your Marriage
No one sets out deliberately to damage his or her...
Read more
Kenyan Government Raises Concerns Over Ford Foundation...
The Kenyan government has written to the Ford Foundation, expressing...
Read more
Rais wa Kenya William Ruto, anayetamatiza ziara...
Ruto ameitoa kauli hii mbele ya rais Biden, kujibu madai...
Read more
SAMIA KUJENGA NYUMBA 5000 ...
Magazeti
See also  MKUU WA MKOA MSTAAFU AKAMATWA KWA ULAWITI
Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
Read more

Leave a Reply