Mwanzo Mwisho wa Maisha ya Ebrahim Raisi kiongozi mkuu wa Iran

0:00

NYOTA WETU

Ebrahim Raisolsadati maarufu kama Ebrahim Raisi aliyekuwa amefikisha miaka 64, alikuwa akipigiwa upatu kuwa mrithi anayeweza kukalia kiti cha Ayatollah Ali Khamenei kama Kiongozi Mkuu, nafasi ambayo ni ya juu kabisa ya kisiasa na kidini katika jamhuri hiyo ya Kiislamu na akitajwa kama mtu mwenye msimamo mkali wa kidini.

Alichaguliwa kuwa rais wa Iran mwaka 2021 kupitia chama cha Front of Islamic Revolution Forces, ambacho kilikuwa ni kambi ya kihafidhina na wakati wa kipindi chake, aliongeza ushawishi wa kikanda akiunga mkono Wanamgambo wa Mashariki ya Kati, ikiwemo kuharakisha mpango wa nyuklia wa nchi hiyo huku akiifikisha Iran kwenye ukingo wa vita na Israeli.

Ingawa alishindwa dhidi ya Rouhani mwaka wa 2017, baadaye mwaka 2021 alishinda uchaguzi wa rais baada ya Baraza la Walinzi la nchi hiyo, taasisi inayoamua ni nani kati ya wagombea hao anaweza kugombea, kuwafuta wagombea 32 wa mageuzi na wenye msimamo wa wastani kabla ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa katiba ya Iran, licha ya kwamba cheo cha rais ni kikubwa na chenye maamuzi ya mwisho, lakini Raisi alikuwa nambari mbili katika muundo wa kimamlaka kwa sababu Ali Khamenei ndiye anayefanya kazi kama mkuu wa nchi na ndiye mwenye uamuzi wa mwisho katika masuala yote ya kimkakati na ni Kamanda mkuu wa Kijeshi ya Iran.

Ebrahim Raisolsadati (Ebrahim Raisi) alizaliwa Desemba 14, 1960 katika familia iliyoshika dini ya Wilayani Noghan, Mashhad Nchini Iran. Baba yake, Seyed Haji, alifariki akiwa na umri wa miaka 5 na alimaliza elimu yake ya msingi katika shule ya Javadiyeh, kisha akajiendeleza huko Hawza (shule ya Kiislamu) na mwaka 1975, alijiunga na Seminari ya Qom, Shule ya Ayatollah Boroujerdi akiwa na miaka 15.

See also  JONAS MKUDE AMSHTAKI MO DEWJI

Akiwa msomi wa kidini katika serikali ya kitheokrasi ya Iran na mfuasi wa Ayatollah Khamenei, Raisi alipanda ngazi nakuwa na nyadhifa katika idara ya mahakama, akihudumu kama Mwendesha Mashtaka katika miji kadhaa, baadaye akateuliwa kuwa jaji mkuu wa Iran, akiaminika kuwa sehemu ya kamati ndogo iliyoamuru kuuawa kwa maelfu ya wapinzani wa kisiasa mwaka 1988.

Aliwahi kushutumiwa kwa miongo kadhaa ya ukiukaji wa haki za binadamu, kiasi ilipelekea kuwa mhusika wa kuadhibiwa vikwazo na Marekani na wakati wa urais wa Raisi, Iran ilikabiliwa na maandamano makubwa dhidi ya serikali baada ya kifo cha mwanamke kijana wa Kikurdi, Mahsa Amini, chini ya ulinzi wa polisi. Mamlaka ilijibu kwa msako mkali uliojumuisha mauaji na mauaji.

Jambo jingine, katika kipindi chake Iran ilipata matukio kadhaa ikiwemo maandamano makubwa dhidi ya Serikali katika miongo kadhaa kutokana na kuzorota kwa uchumi kwa sababu ya vikwazo vya kimataifa na ukosefu mkubwa wa ajira, ikiwemo ghasia wakati wa kifo cha Msichana wa Kikurdi wa Irani, Mahsa Amini aliyefariki mikononi mwa Polisi baada ya kukamatwa kwa kukiuka kanuni za mavazi ya Kiislamu.

Vita vya kivuli vya miaka mingi na Israel vilianza wazi hivi karibuni, baada ya Iran kurusha mamia ya makombora na ndege zisizo na rubani huko Israel, shambulio lilitokana na kuongezeka kwa mvutano kati ya nchi hizo mbili baada ya Hamas, kundi la wanamgambo linaloungwa mkono na Iran, kuvamia Israel Oktoba 7.

Katika kipindi hicho, Iran pia imeibuka kama msambazaji wa kigeni wa Urusi wa ndege zisizo na rubani za kijeshi na ikumbukwe pia mwaka jana 2023 Iran ilifanya makubaliano na Saudi Arabia na kurejesha uhusiano wa kidiplomasia, hivyo hali hii ilipelekea Raisi kukabiliwa na mvutano, baada ya kuonekana wazi akiiunga mkono Urusi kimya kimya.

See also  Steve Cooper Happy to have "positive " Patson Daka back in the mix

Katika ripoti ya Umoja wa Mataifa, Rais alitajwa katika Mahakama ya Iran ambayo iliidhinisha kunyongwa kwa angalau watoto tisa kati ya mwaka 2018 na 2019, huku akikosolewa vikali kwa jinsi ilivyoshughulikia kuwekwa kizuizini kwa kwa Mahsa Amini, hali iliyoibua utata kwani ilipelekea kifo chake na kusababisha maandamano makubwa nchini kote mwishoni mwa 2022.

Mei 19, 2024 Rais Ebrahim Raisi (63), Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo, Amir Abdollahian na Maafisa wengine saba waliokuwamo kwenye msafara walipata ajali ya Helikopta na baadaye kupatikana wakiwa wamefariki katika eneo la ajali la Jolfa, lililopo zaidi ya kilomita 600 kutoka Tehran karibu na mpaka wa jimbo la kaskazini-magharibi mwa Azerbaijan wakati wakitokea katika mkutano na Rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Iran la Mehr la Nchini Iran, liliripoti kuwa, Helikopta hiyo ilitoweka kwenye rada Jumapili mchana na katika ajali hiyo hakuna mtu aliyenusurika na Serikali ya Iran haikutia neno kuhusiana na tukio hilo, huku Mkuu wa shirika la Hilali Nyekundu la Irani, Pirhossein Koolivand akisema timu za waokoaji ziliyafikia mabaki ya helikopta hiyo na kudai kuwa hali mbaya ya hewa ilichangia kutatiza shughuli za uokozi.

Kufuatia kifo hicho, Kiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei Mei 20, 2024 akamteua Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran, Mohammad Mokhber kuwa rais kwani kwa mujibu wa katiba ya Iran, makamu wa kwanza wa rais atachukua wadhifa huo iwapo rais atafariki, kuondolewa madarakani, kujiuzulu au kuwa mgonjwa kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili.

Raisi ameacha mjane Jamileh Alamolhoda, binti wa Imamu wa Swala ya Ijumaa ya Mashhad, Ahmad Alamolhoda ambaye ni Profesa mshiriki katika Chuo Kikuu cha Shahid Beheshti cha Tehran na rais wa Taasisi ya Mafunzo ya Msingi ya Sayansi na Teknolojia ya chuo hicho, wakibahatika kupata watoto wawili wa kike na wajukuu wawili.

See also  MTANGAZAJI KAPINGA KISAMBA CLARISSE AWEKA REKODI HII

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

TV presenter Laura Woods has revealed she...
They each won gold in their respective weight divisions at...
Read more
MAJOR REASONS WHY RELATIONSHIP END
LOVE TIPS ❤ 6 MAJOR REASONS WHY RELATIONSHIPS ENDAre you...
Read more
A DIFFERENCE BETWEEN A COMPANY PROFILE &...
BUSINESS PLAN A business plan is a written document that outlines...
Read more
WATANZANIA WAFUNGASHIWA VIRAGO ARMENIA 🇦🇲
MICHEZO Klabu ya West Armenia inayoshiriki ligi kuu ya Armenia...
Read more
Usajili wa Chama Yanga wamuibua Molinga
Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, David Molinga amesema kuwa uamuzi alioufanya...
Read more

Leave a Reply