SHUHUDIA SHUGHULI YA MAZISHI YA EBRAHIM RAISI KIONGOZI WA IRAN

0:00

HABARI KUU

Raia wengi wa Iran wamejitokeza katika mji mkuu wa nchi hiyo Tehran, kushiriki katika mazishi ya kitaifa ya Rais Ebrahim Raisi.

Rais huyo wa Iran akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Hossein Amir – Abdollahian pamoja na maafisa wengine sita wa ngazi ya juu, walifariki dunia baada ya helikopta waliyokuwa wakisafiria kuanguka karibu na eneo la mpaka wa Iran na Azerbaijan.



Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei ataongoza dua mjini Tehran kabla ya majeneza yaliyobeba miili ya viongozi hao kupelekwa katika uwanja mkubwa wa Azadi, ambapo yatafanyika mazishi hayo ya kitaifa.

Picha mbalimbali za video zilizorushwa kupitia kituo cha televisheni cha Serikali ya Iran zimeonyesha mitaa mbalimbali ya Tehran ikiwa imejaa waombolezaji, wengi wao wakiwa wamebeba picha ya Rais Raisi na wengine wakiwa wameshika bendera za Taifa hilo.



Viongozi kutoka mataifa mbalimbali wamethibitisha kushiriki kwenye mazishi hayo ya kitaifa ya Rais huyo wa Iran.

Baada ya mazishi hayo ya kitaifa mjini Tehran, mwili wa Rais Ebrahim Raisi utasafirishwa kwenda jimbo la Khorasan ambalo lipo kusini mwa Iran na baadae nyumbani kwake Mashhad kwa ajili ya mazishi rasmi yatakayofanyika kesho Alhamisi Mei 23, 2024.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Rais wa Nigeria Bola Tinubu amepiga marufuku...
Hatua ya Rais inafuatia uwepo wa malalamiko ya Wananchi wanaodai...
Read more
ZUCHU AFUNGIWA KUFANYA MZIKI
NYOTA WETU Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la...
Read more
Presidential jet: Tinubu, NASS, political class now...
Former Minister of Education, Oby Ezekwesili, has said President Bola...
Read more
Meru Governor Granted Temporary Reprieve as High...
The High Court in Nairobi has issued conservatory orders suspending...
Read more
SPIKA TULIA NA MKONO WA CHUMA WA...
MAKALA
See also  I’m not preoccupied with 2027 presidency – Atiku replies Bode George
Luhaga Mpina ameeleza umma, maamuzi ya mawaziri, Hussein Bashe...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply