AHUKUMIWA KIFUNGO MAISHA JELA KWA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 13

0:00

HABARI KUU

Mahakama ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga imemuhukumu kwenda jela kifungo cha maisha Ramadhani Bakari Iddi (46) mkazi wa Kilapula kata ya Ngomeni Wilayani hapo kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 13.

Akitoa hukumu hiyo leo hii Hakimu mkazi wa mahakama ya Wilaya hiyo Mh. Geofrey Haule amesema kwamba mahakama imemtia hatiani mshtakiwa huyo kwakuwa mnamo tarehe 08/11/2023 mshtakiwa alitenda kosa hilo la kumlawiti mtoto huyo pindi alipomlubuni na kisha kwenda naye makaburini kwa lengo la kumtoa mashetani ndipo akafanya kitendo hicho cha kinyama kwa dhamira ovu.

Amesema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hivyo mahakama imejiridhisha pasi na shaka kuwa mshtakiwa ndio mtenda kosa hilo hivyo Mahakama inamuhukumu mshtakiwa kutumikia kifungo cha maisha Jela ili iwe fundisho katika jamii.

Aidha hakimu Haule amesema kwamba adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kifungu cha sheria 154 (1)(a) na 2 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 RE.2022.

Awali baada ya hukumu hiyo kutolewa wakizungumza kwa nyakati tofauti waendesha mashtaka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilayani Muheza Inspector Joseph Njama na CPL Michael Msangawale waliishukuru Mahakama kwa kutoa adhabu hiyo kali kwa mtuhumiwa huyo na huku wakiongeza kusema kuwa inaenda kuwa fundisho kwa wale wote wenye nia ovu ya kutenda makosa hayo katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

21 HABITS THAT TURNS BOYS INTO MEN
LOVE TIPS ❤ 1. Responsibility:Take responsibility for your actions &...
Read more
KAGAME NI KAMA HITLER ...
HABARI KUU. Rais wa DRCONGO ,Felix Tshisekedi ametoa kauli ya...
Read more
Mfahamu Didi-Stone mmoja wa watoto 7 wa...
NYOTA WETU
See also  Kiongozi wa upinzani Nchini Israel Yair Lapid ametoa wito kwa Waziri Mkuu wa taifa hilo Benjamin Netanyahu, kuzingatia mpango uliotangazwa na rais wa Marekani Joe Biden wa kusitisha mapigano Gaza.
Didi-Stone Olomidé ambaye amepewa jina kutokana na mjomba...
Read more
EMILIO NSUE LOPEZ AMETANGAZA KUSTAAFU SOKA ...
MICHEZO NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Guinea ya Ikweta,...
Read more
Kwanini Daraja la Magufuli (Kigongo-Busisi) limechelewa kutumika...
Daraja la John Magufuli (Kigongo- Busisi) lenye urefu wa...
Read more

Leave a Reply