Motsepe: Goli la Aziz Ki lilikuwa halali

0:00

8 / 100

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Patrice Motsepe amesema goli walilofunga Yanga SC dhidi ya Mamelodi Sundowns lililokataliwa lilikuwa halali.

Motsepe amesema hayo leo visiwani Zanzibar alipowasili kwa ajili ya kushuhudia michezo ya fainali ya mashindano michuano ya soka kwa shule za Afrika (African Schools Football) ambazo zitachezwa leo katika Uwanja wa New Amaan.

Amesema kuwa yeye kama Rais wa CAF hakupaswa kutoa maoni lakini “kama shabiki wa mpira, nilipotazama, lilikuwa ni goli.”

Kufuatia kukataliwa kwa goli hilo, timu hizo zilimaliza michezo yote miwili ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika bila kufungana, na Yanga ikatolewa kwa mikwaju ya penati baada ya kufungwa penati 3-2.

Katika fainali hizo, timu ya soka ya wavulana ya Tanzania itacheza dhidi ya Guinea, huku upande wa wasichana Morocco itakutana na Afrika Kusini.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

President Bola Tinubu has arrived in Accra,...
The President departed Abuja on Saturday morning and was received...
Read more
Mahakama Yatupilia Mbali Maombi ya Mjane wa...
Mahakama ua Rufani imetupilia mbali shauri la maombi ya marejeo...
Read more
Enzo Fernandez aomba Radhi kwa Ubaguzi Michezoni
Klabu ya Chelsea imeingia kwenye sintofahamu baada ya kiungo Enzo...
Read more
RAIS TSHISEKEDI KUMPA ZAWADI LUVUMBU NZINGA
MICHEZO Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi...
Read more
Hamisa Mobetto na Aziz Ki je ni...
Baada ya Taarifa kusambaa Mitandaoni kuhusiana na Hamisa Mobetto ambaye...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  FERRAN TORRES AMZAWADIA MAREHEMU ZAWADI

Leave a Reply