Ruto ameitoa kauli hii mbele ya rais Biden, kujibu madai kuwa Kenya, imesukumwa na Marekani kuwapeleka polisi wake zaidi ya Elfu 1 kusaidia kurejesha utulivu jijini Port au Prince.
Kutumwa kwa polisi wa Kenya kuongoza kikosi cha Kimataifa kusaidia kuleta utulivu nchini Haiti, unakabiliwa na upinzani kutoka Mahakamani, kutokana na chama cha upinzani cha Third Way Alliance kupinga mpango huo, unaosema ni kinyume cha Katiba.
Rais wa Marekani, Joe Biden, amesema nchi yake itahakikisha Kenya inakuwa mwanachama wa jumuiya ya nchi za kujihami za magharibi NATO, hatua ambayo itaifanya Kenya kuwa taifa la kwanza kwenye ukanda wa jangwa la Sahara kuwa mwanachama.
Katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Marekani, rais Ruto, aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kutetea demokrasia na usalama wa ukanda na dunia.