Kwanini Patrice Motsepe alisema goli la Young Africans lilikuwa halali?

0:00

4 / 100

Ijumaa iliyopita Asubuhi Rais wa CAF, Patrice Motsepe alikuwa katika ardhi ya Tanzania Visiwani Zanzibar. Motsepe alikuja kwa ajili ya Mashindano ya Fainali za African Schools Football.

Baadae muda mfupi tukaona stori ikitembea mitandaoni kuwa Motsepe amekubali bao alilofunga Stephane Aziz KI pale kwa Madiba dhidi ya Mamelodi Sundowns lilikuwa bao halali.

Ni kichekesho, Kwanini Motsepe atoe kauli hii leo? Kauli yake haina madhara yoyote kwa sasa, zaidi inawapaka @yangasc mafuta kwa mgongo wa chupa.

Afrika ilisema, Yanga SC nao waliandika hadi barua kuhusu bao kukataliwa. Kila mmoja alichafukwa kwa kilichotokea usiku ule, lakini barua ya Yanga SC nayo isingeweza kubadili uamuzi wa kiwanjani.

Maisha yalikuwa hivi. Vitu vingi vimepita hapa kati baada ya mechi ile ya Afrika Kusini. Juzi Motsepe amekuja kuishitua mioyo iliyolala. Sijui aliulizwa swali au aliamua ‘kujiropokea’ zake.

Sijui kwanini Motsepe alifanya vile. Kinachomuhukumu Motsepe ni kitu kimoja tu. Nafasi yake ya Urais ndani ya CAF na nafasi yake kama kiongozi wa juu wa Mamelodi Sundowns.

Motsepe amekasimu madaraka yake kwa mtoto wake pale Mamelodi, lakini nyuma ya pazıa ni rahisı hivyo? Mashaka yanaingia unapojua tuko Afrika.

Ni kweli Motsepe hana ushawishi na chochote ndani ya Mamelodi? Swali ni gumu. Jibu lake ni jepesi tu. Afrika bado hatuna utaratibu wa kuachia madaraka na kuacha kufuata guata kwa nyuma.

Mbele ya pazia ni kweli Motsepe hafanyi kazi zozote za Mamelodi. Hii ni nyuma ya pazia, lakini nyuma ya pazia bado Motsepe ana nguvu na ushawishi mkubwa na muda mwingine huenda akawa anapiga hadi simu kuulizia mambo yanavyokwenda.

See also  Azam yanasa mbadala wa Fei Toto kutoka Ivory Coast

Kiufupi tu, Motsepe ameamua kusema tunachopenda kukisikia. Watanzania wanapenda vile. Kuna Watanzania wameondoka na kauli ile na kusahau kila kitu.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

FANYA MAMBO HAYA ILI KUTUNZA UKE WAKO...
MAPENZI. Utunzaji wa sehemu ya siri ya Mwanamke (uke) ni...
Read more
MATURE WAY OF BEING IN A RELATIONSHIP
LOVE TIPS ❤ 1. BE PATIENT WITH YOUR PARTNER: Avoid...
Read more
15 THINGS YOU MUST GIVE YOUR SPOUSE...
Do you really desire a healthy marriage? Are you really sure? Are...
Read more
The Premier League have officially announced the...
The Nike Flight Premier League ball will enjoy its first...
Read more
MADHARA YA KUVUTA SHISHA KWA BINADAMU ...
Makala Kwa mujibu wa utafiti wa Taasisi ya American Lung Association...
Read more

Leave a Reply