Lengo la Uenyekiti huo ni kuhamasisha amani miongoni mwa watanzania bila kubagua dini, Madhehebu, mila, Viongozi wa Chama na serikali, Wabunge na wananchi kuanzia ngazi ya mtu mmoja, familia hadi taifa.
Makabidhiano hayo yanefanyika kwenye hafla fupi jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya na Mashirikisho ya Amani ya dini, madhehebu mbalimbali nchini na Viongozi wa kimila.
Akimkabidhi barua ya utambulisho wa nafasi hiyo ya Uenyekiti Balozi wa shirikisho la amani duniani bara la Afrika ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Amani duniani Kanda ya Afrika UPF kutoka nchi ya Ivory coast Adama Doumbia amesema UPF ni Shirika lisilo la Kiserikali (NGO) ambayo kazi yake kubwa ni kutangaza na kusimamia amani baina ya watu wa dini zote na makabila yote na nyanja zote ambalo Makao makuu yake ni nchini Korea.
Aidha, Adama ameagiza kuandaliwa kwa sherehe kubwa Maalum ya kumtambulisha Mwenyekiti huyo mpya wa Shirikisho hilo la Amani nchini Tanzania ambaye atakabidhiwa rasmi na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mama Marie Kigalu ambapo Viongozi mbalimbali watahudhuria.