Ni mazingira yapi Rais wa Tanzania anaweza kulivunja Bunge ?

0:00

4 / 100

Kwa mujibu wa Ibara ya 90(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Tanzania atavunja Bunge, kunapotokea kati ya yafuatayo;

(a) Kama Bunge limemaliza muda wa uhai wake kwa mujibu wa ibara ya 65 ya Katiba au wakati wowote katika miezi kumi na miwili ya mwisho ya uhai wa Bunge, isipokuwa tu kama Spika amepokea taarifa rasmi inayopendekeza kuundwa kwa Kamati Maalum ya Uchunguzi kwa madhumuni ya kumwondoa Rais madarakani kwa mujibu wa ibara ya 46A ya Katiba

(b) Kama Bunge limekataa kupitisha Bajeti iliyopendekezwa na Serikali

(c) Kama Bunge limekataa kupitisha muswada wa sheria kwa mujibu wa ibara ya 97(4) ya Katiba

(d) Kama Bunge limekataa kupitisha hoja ambayo ni ya msingi katika sera za Serikali, na Rais anaona kwamba njia ya kuendelea kutoka hapo si kumteua Waziri Mkuu mwingine bali ni kuitisha Uchaguzi Mkuu

(e) Endapo, kutokana na uwiano wa uwakilishi wa vyama vya siasa katika Bunge, Rais anaona kwamba hakuna uhalali kwa serikali iliyopo kuendelea kuwapo, na wala haiwezekani kuunda Serikali mpya.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  ALI BONGO BAADA YA KUPINDULIWA HAWA MAARUFU
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading