Mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki kiwanda bunu cha kutengeneza na kusambaza pombe kali bandia, Frank Donatus Mrema na wenzake wawili aliokuwa amewaajiri katika kiwanda hicho, wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela, huku mmoja akimwaga shukrani kwa Mungu na Mahakama baada ya kutiwa hatiani.
Frank na wenzake hao, Faham Salim Ngoda na Issa na Issa Juma Hassan walihukimiww adhabu hiyo jana mahama ya Hakimu Mkazi Kivukoni (Kinondoni), baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kukutwa na kemikali hatarishi aina ya Ethanol isivyo halali, katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili.
Walikuwa wakitumia kemikali hiyo kutengenezea vileo vikali aina ya K-vant, Double Kick na Smart Gin na kisha kubandika stika za Mamlaka ya Mapyo Nchini (TRA) na nembo bandia za kampuni zinazozalisha vileo hivyo.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Veneranda Kaseko. Ambapo baada ya kusomewa adhabu hiyo walipewa fursa ya kujitetea, ndipo Issa akaanza kwa kutoa Shukrani kwa Mungu kwa kumfikisha siku hiyo na kumuwezesha kufika mahamani hapo na kueleza kuwa huo ni uamuzi sahihi wa mahakama dhidi yake.
“Mheshimiwa hakimu, nipende kuishukuru siku hii ya leo na Mwenyezi Mungu mpaka kufika hapa na nipende kuishukuru Mahakama kwa kutoa uamuzi huu sahihi kwangu japokuwa inaniuma kwa kuwa si mtendaji ila niombe mahakama inipunguzie adhabu.” Amesema Issa.