Mshambuliaji na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe amesema yupo tayari kuianika hadharani Klabu atakayoitumikia msimu ujao 2024/25.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, amewaacha njia panda mashabiki wake, ambao wanatamani kufahamu wapi atakapocheza msimu ujao, Licha ya Miamba ya Soka mjini Madrid- Hispania Real Madrid kutajwa kuwa kwenye nafasi nzuri ya kumsajili katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.
Mbappe ameweka wazi mpango huo alipohojiwa na Kituo cha Televisheni cha CNN cha nchini Marekani, ambapo amesema muda si mrefu wataweka kila kitu hadharani.
“Klabu yangu ijayo itakuwa hadharani hivi karibuni, ni suala la muda tu. Nimefurahia sana, na ninaendelea kuwa na furaha kwa hatua nitakayopiga.
“Inabidi mashabiki wangu waendelee kusubiri kwa sababu sio siuku nyingi sana zilizosalia, kabla sijatangaza maamuzi yangu binafsi.”