Stormy Daniels ndilo jina la mwanamke aliyetawala katika kesi ya jinai ambayo Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump alipatikana na hatia katika kesi ya kihistoria iliyofanyika Manhattan.
Jina lake halisi ni Stephanie Gregory Clifford, mwigizaji wa zamani na mkurugenzi wa filamu za wakubwa. Katika kesi hiyo anadai kuwa mwaka 2006 alikutana na Trump, wakati tayari alikuwa ameoana na mke wake wa sasa, Melania, kitu ambacho mara kwa mara Trump alikanusha.
Majaji wa mahakama ya New York wameonekana kumwamini na hivyo kumpata rais huyo wa zamani wa Marekani na hatia ya mashtaka 34 yanayohusiana na kughushi taarifa za uhasibu ili kuficha malipo ambayo wakili wa Trump angemlipa mwanamke huyo ili kununua ukimya wake kuhusu uhusiano huo na hivyo kumlinda katika kampeni za uchaguzi za mwaka 2016 ambazo Trump alishinda urais.
Stephanie alizaliwa Baton Rouge, katika jimbo la kusini la Louisiana, mwaka wa 1979, na ni mpenzi wa kuendesha farasi.
Akiwa mtoto, ndoto yake ilikuwa kuwa daktari wa mifugo, lakini baada ya talaka ya wazazi wake akiwa na umri wa miaka minne, alilelewa na mama yake ambaye alikuwa na wakati mgumu kumsomesha.
Katika umri wa miaka 17 alianza kufanya kazi kama mcheza dansi katika vilabu vya usiku.
Mwaka 2000 alianza kazi yake kama mwigizaji wa filamu za watu wazima na kampuni ya utengenezaji wa Wicked Pictures.