Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema kuwa kinachoendelea katika Uchaguzi Mkuu nchini Afrika Kusini ambapo Chama Tawala cha ANC kimeshindwa kupata kura za kuunda serikali peke yake inapaswa kuwa somo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

0:00

9 / 100

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumamosi Juni 01, 2024 na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi, Mahusiano na Umma wa ACT Shangwe Ayo, Shaibu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho mkoani Pwani katika kikao kilichofanyika kata ya Mwandege, Jimbo la Mkuranga Jumamosi.

“Kinachotokea kwa ANC nchini Afrika Kusini kinapaswa kuwa funzo kwa CCM kuwa ukipuuza hisia za wananchi, nao watazungumza kupitia sanduku la kura. Kwa mara ya kwanza tangu kushika serikali mwaka 1994, ANC imeshindwa kufikisha 50% ya kura ili kuunda serikali. Uchambuzi unaonesha hii ni ishara na matokeo ya ANC kushindwa kuwajibika kwenye masuala muhimu ya wananchi kama ukosefu wa ajira, huduma mbovu ya umeme, ufisadi na utawala mbovu” Amenukuliwa Shaibu katika taarifa hiyo.

Aidha Shaibu ameendelea kusema kuwa siku za CCM kutawala zinahesabika kwani imepuuza kwa kiasi kikubwa hisia za Watanzania.

“Mfano, uchambuzi wetu wa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) unaonesha kuwa fedha za umma, za wananchi wa Tanzania kiasi cha Tsh. Trilioni 3.14 zimepotea kwa sababu ya ubadhirifu na hakuna hatua yoyote ya maana iliyochukuliwa dhidi ya ubadhirifu huo” Ameongeza Shaibu.

Katika hatua nyingine, Ado Shaibu amesema kwamba chama cha ACT kinawasiliana na asasi mbalimbali za kiraia kufungua kesi mahakamani kuhakikisha kwamba uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa unasimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi badala ya Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MANCHESTER HAINA MPANGO NA SOFYAN AMRABAT ...
MICHEZO
See also  WIVES WHO CAN'T HANDLE THE TRUTH
Klabu za AC Milan na Juventus zinaangalia uwezekano wa...
Read more
McLaren taking nothing for granted with constructors'...
LAS VEGAS, - McLaren are on the verge of winning...
Read more
MARAIS 10 WA AFRIKA WALIOFIA MADARAKANI ...
MAKALA Baada ya siku ya leo nchi ya Namibia 🇳🇦...
Read more
YANGA YAINGIZA PESA NDEFU KWENYE TAMASHA LAKE...
Dar es salaam. Matamasha ya Wiki ya Mwananchi na Simba...
Read more
WATU 22 WAFARIKI MGODINI GEITA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Leave a Reply