Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza kuwa hakutakuwa na usitishaji vita ya kudumu huko Gaza hadi pale uwezo wa kijeshi na uongozi wa Hamas utakapoangamizwa na mateka wote waachiliwe.

0:00

10 / 100

Kauli yake inafuatia baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kutangaza kuwa Israel imependekeza mpango wa hatua tatu kwa Hamas unaolenga kufikia usitishaji vita ya kudumu.

Mwanasiasa mkuu wa Hamas ameliambia shirika la BBC kuwa “itakubali makubaliano haya” ikiwa Israel itafanya hivyo.

Mazungumzo hayo yanakuja huku mapigano yakiendelea huko Rafah, kukiwa na ripoti za mashambulizi ya anga ya Israel siku ya Jumamosi katika mji huo ulio kwenye mpaka wa Misri na Gaza.

Hakuna hakikisho kwamba shinikizo la umma la Bw Biden kwa Israel na Hamas kuukubali mpango huo litachochea makubaliano.

Katika taarifa yake siku ya Jumamosi, ofisi ya Bw Netanyahu ilisema kuwa “masharti ya Israel ya kumaliza vita hayajabadilika”.

Amesema “kuharibiwa kwa uwezo wa kijeshi na kiutawala wa Hamas, kuachiliwa kwa mateka wote na kuhakikisha kuwa Gaza haileti tishio tena kwa Israel”.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Israel “itaendelea kusisitiza masharti haya yatimizwe” kabla ya kukubaliana na usitishaji wa kudumu wa mapigano, na kusisitiza kwamba hakuna makubaliano yanayoweza kusainiwa kabla ya kufikiwa kwa hayo kwanza.

Siku ya Ijumaa, Bw Biden alielezea mpango huo kama pendekezo la kina la Israel ambalo lilifungua njia ya usitishaji wa kudumu wa mapigano.

Awamu ya kwanza itajumuisha usitishaji vita kamili, kuondolewa kwa vikosi vya Israel kutoka maeneo yenye watu wengi na kubadilishana baadhi ya mateka kwa wafungwa wa Kipalestina.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SUALA LA PACOME NA CAREN SIMBA LIKO...
NYOTA WETU Mrembo Caren Simba amejikuta kwenye wakati mgumu wa...
Read more
Nape Nnauye Ameponzwa na Mdomo au Utendaji...
MAKALA
See also  SASA NI RASMI MWEZI WA RAMADHAN UNAANZA MACHI 12
Usiku wa kuamkia leo Jumatatu tumefikiwa na taarifa za kutoka...
Read more
President Ruto's Behind-the-Scenes Meetings Precede Major Security...
President William Ruto has announced a series of leadership changes...
Read more
AHUKUMIWA MAISHA JELA KWA KUMLAWITI MTOTO WA...
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Lindi, imemuhukumu Mohamed Said...
Read more
AMUUNGUZA MTOTO WAKE WA MIAKA MIWILI KWA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply