Rais Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) kwenye sekta ya anga, iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Anga cha Korea Kusini.
Akizungumza mara baada ya kutunukiwa shahada hiyo Rais Samia amesema Tanzania inatambua umuhimu wa sekta ya usafiri wa anga na kwamba jiografia imekuwa msingi wa kukuza sekta ya usafiri wa anga.
Ameongeza kuwa sekta hiyo ni muhimu katika ukuaji wa sekta nyingine huku akibainisha kuwa Serikali ya Tanzania iko kwenye majadiliano na mashirika mengine ya ndege ili yaanze kufanya safari zake nchini Tanzania.
Rais wa Chuo Kikuu cha Anga cha Korea Kusini, Heeh Young Hurr amesema Rais Samia ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kupitia uongozi wenye maono ambao umefanikisha ujenzi wa viwanja wa ndege na maendeleo ya miundombinu ambayo yamechangia ukuaji wa uchumi na kwamba chuo hicho kipo tayari kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali.
Chuo hicho kimesema kimeamua kumtunuku shahada hiyo Rais Samia kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha usafiri wa anga nchini Tanzania.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.