Aliyekuwa mgombea wa kanda ya Nyasa ya Chadema, Mchungaji Peter Msigwa amekata rufaa katika chama hicho, akidai ushindi alioupata Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ haukuwa halali na kulikuwa na mbinu chafu dhidi yake.

0:00

9 / 100

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Juni 3, 2024 Mkoani Iringa, Msigwa ameonesha kutokubaliana na matokeo akidai kuwa hawezi kushindwa uchaguzi.

“Mimi siwezi kushindwa, mimi uchaguzi huu (Uchaguzi wa uongozi wa CHADEMA kanda ya Nyasa) sikushindwa, tumemchagua mwenyekiti wa uchaguzi anaitwa Ayubu Sikagonamo ni mwenyekiti wa wilaya kule wilaya ya Momba alikuwa timu yetu tukashinda, yule mwenyekiti ndiye ambaye huwa anatoa kura ya turufu, tukashinda kwa tofauti ya kura 59 kwa 49 tulikuwa mbele sisi kura 10 pungufu ya kura tatu ambazo hawakuziruhusu zingejumlisha na hiyo moja ambayo walimpa Vitus (Vitus Nkuna, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA kanda ya Nyasa) ushindi ambao hastahili, tuliposhinda tunapotaka kuanza uchaguzi upande wa wenzetu wakiongozwa na Mungai (Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai) wakaanza kuleta fujo kutaka wajumbe wa Makete waondoke kwamba siyo halali”

Aidha Msigwa amedai kuwa kuna rushwa zilitolewa ili asishinde uchaguzi akidai kuna watu walipewa rushwa ya laki 5 mpaka milioni moja.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Mambo Usiyoyajua Kuhusu chura
USIYOYAJUA KUHUSU CHURA HAYA HAPA Chura ni miongoni mwa viumbe wasipendwa...
Read more
KIKWETE NA MUSEVENI WATETA
HABARI KUU Rais wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa...
Read more
YANGA YAINGIA MKATABA WA MILIONI 300 ...
MICHEZO Klabu ya Yanga imeingia Mkataba wenye thamani ya Tsh...
Read more
HERSI AMALIZA UVUMI WA PACOME
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
YANGA YATOA UFAFANUZI KUHUSU SAKATA LA KUFUNGIWA...
MICHEZO
See also  VYAMA 11 VYA LAANI KAULI YA TUNDU LISSU
“Kabla ya Dirisha la usajili kufunguliwa sisi Yanga tulikuwa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply