Licha ya msimu ujao Simba sc kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika, lakini wataanzia katika mzunguko wa pili wa michuano hiyo, huku Yanga sc watakaocheza Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika nao wakianzia hatua hiyo.

0:00

9 / 100

Mashindano ya CAF msimu wa 2024/25 yataanza kwa raundi ya awali kati ya Agosti 16 hadi 18 Agosti, 2024 huku hatua za makundi zikipangwa Oktoba hadi mwezi Desemba mwaka 2024.

Klabu ya Yanga SC itaanza kampeni zake za Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye raundi ya pili michuano hiyo na wataanzia ugenini huku Simba Sc ikianzia raundi ya pili ya kombe la Shirikisho Afrika nayo itaanzia ugenini.

Licha ya Azam FC kusiriki Klabu Bingwa, lakini wao wataanzia raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Coastal Union wakianzia raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika.

Azam FC na Coastal Union wataanzia nyumbani kwenye michuano hiyo. Tanzania ni miongoni mwa nchi 12 za Afrika zitakazoingiza timu nne kwenye mashindano ya CAF.

Nchi nyingine ni Algeria, Angola, Ivory Coast, Misri, Libya, Morocco, Nigeria, DR Congo, Afrika Kusini, Sudan na Tunisia.

Usajili wa wachezaji watakaoshiriki katika hatua ya awali utafanyika kati ya tarehe Julai 1, 2024 hadi Julai 20, 2024.

Usajili wa wachezaji watakaoshiriki katika hatua ya pili utafanyika kati ya tarehe Julai 21 hadi Agosti 31, 2024.

Usajili wa wachezaji watakaoshiriki katika hatua ya makundi utafanyika kati ya Septemba 1 hadi Septemba 30, 2024.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SABABU BILIONEA HARRY ROY VEEVERS KUTOKUZIKWA KWA...
HABARI KUU MJANE wa marehemu Harry Roy Veevers, raia wa...
Read more
Prominent Kenyan Journalist Abducted from Police station...
On the morning of Wednesday, July 17th, veteran Kenyan journalist...
Read more
Uke Wenye Afya bora hauna Harufu wala...
🍂Utunzaji wa uke ni jambo la muhimu sana kwa mwanamke....
Read more
CHELSEA KUVUNJA REKODI KWA OSIMHEN
MICHEZO
See also  50 CENT BADO ANAMSHAMBULIA MICHAEL JACKSON
Bosi wa klabu ya Chelsea, Toddy Boehly , amedhamiria...
Read more
President Bola Tinubu on Friday in Beijing...
Addressing members of Nigerians in Diaspora Organization in China (NIDO...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply