SIASA
Tume Huru ya uchaguzi nchini Rwanda imewaidhinisha watu watatu katika kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu ujao mwezi Julai.
Paul Kagame kutoka chama cha FPR , Frank Habineza wa chama cha Democratic Green Party na Philippe Mpayimana mgombea binafsi ndio walioidhinishwa na tume huye licha ya Rais Paul Kagame kupewa nafasi kubwa na kushinda tena uchaguzi.
Ambao waliondolewa kwa kushindwa kuonyesha vyeti vyao halali vya kuzaliwa na wadhamini ambao hawajatimiza matakwa ya tume wanaweza kukata rufaa ndani ya siku tano.
Wagombea sita kati ya tisa waliokuwa wamepeleka vyeti vyao ndio ambao wamekutwa wakiwa hawajakidhi vigezo vya kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwezi Julai 15,2024.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.