Narendra Modi ameapishwa kuhudumia India kwa muhula wa tatu akiwa amepata ushindi mdogo

0:00

Mwanasiasa mkongwe Narendra Modi (73), leo amekula kiapo mbele ya Rais Draupadi Murmu wa India kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo kwa muhula wa tatu katika sherehe kubwa iliyofanyika Ikulu.

Katika sherehe hiyo Mawaziri wa Baraza jipya nao waliapishwa. Jiji la Delhi lilikuwa na ulinzi mkali, huku Ikulu ikizungukwa na zaidi ya askari Polisi 2,500, na hakuna Ndege iliyoruhusiwa kuruka ama kupita.

Modi ameahidi kuongoza kwa haki bila upendeleo wala ubaguzi, na amesema kuwa kipaumbele chao ni kuwawezesha masikini na watu wa tabaka la kati.

Maelfu ya wageni walihudhuria sherehe hizo wakiwemo viongozi kutokea nchi za jirani kama Bangladesh, Nepal,Sri Lanka na Maldives.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MAGARI YENYE THAMANI KUBWA DUNIANI
MAKALA 1.Rolls-Royce Droptail inaongoza katika orodha ya magari yanayouzwa bei...
Read more
10 THINGS YOU MUST DISCUSS IN COURTSHIP
LOVE TIPS ❤ 1. WHERE ARE YOU GOING TO LIVE...
Read more
MESSI NA RONALDO KUKUTANA UWANJANI
MICHEZO Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kukutana tena February mwakani...
Read more
KOREA KASKAZINI YAWEKA SHERIA YA ULAJI NYAMA...
Korea Kaskazini imepiga marufuku wananchi wake kufuga mbwa na kuishi...
Read more
7 WAPOFUKA MACHO WAKITIBU RED EYES KIENYEJI...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
See also  Inter's Inzaghi regrets missed opportunities in Monza draw

Leave a Reply