Kabla hujafikiria kutoa mimba, ni muhimu kufahamu matokeo mabaya kiafya yanayoweza kujitokeza siku za mbele baada ya kufanya kitendo hichi, hasa kwenye swala zima la uzazi.
NINI KINATOKEA BAADA YA KUTOA MIMBA?
-Wanawake wengi hupata dalili hizi siku chache baada ya kutoa mimba, dalili ambazo zinaweza kuchukua mpaka siku 21 kuisha
1.kutokwa damu kwa week 2 mpaka 4
2.muumivu ya nyonga
3.mwili kukosa nguvu na kusinzia ovyo
4.kutapika na kizunguzungu
MADHARA MAKUBWA YANAYOWEZA KUJITOKEZA BAADA YA KUTOA MIMBA NI PAMOJA NA:
▫️majeraha kwenye mlango wa kizazi na kizazi
▫️kutokwa damu kupita kiasi mpaka kuishiwa damu
▫️mimba kushindwa kutoka yote(incomplete abortion) na hivo kuhitaji upasuaji mwingine
▫️maambukizi sugu kwenye via vya uzazi(PID)
▫️makovu kwenye tumbo la uzazi
▫️kufanyika kwa mashimo ndani ya kizazi
▫️mgonjwa kufariki
MADHARA YA MUDA MREFU BAADA YA KUTOA MIMBA
▫️kujifungua mtoto kabla ya muda wake kutimia(pre-term deliveries
▫️kutoa mimba husababisha kulegea kwa mlango wa kizazi na hivo kuongeza hatari ya mimba zijazo kutoka ama kujifungua kabla ya wakati yaani chini ya week 37.
endapo mtoto atazaliwa chini ya muda wa week 37 anaweza kupata madhara ya kiafya kama matatizo ya ubongo.
▫️saratani ya matiti: Tafiti zinasema kwamba kutoa mimba kunaongeza hatari ya mwanamke kupata saratani ya matiti.
kuugua magonjwa sugu kama chlamydia na PID
▫️kupata magonjwa ya akili:
tafiti zinasema kwamba waawake wengi hupata matatizo ya akili baada ya kutoa mimba na dalili kama kujutia kutoa mimba
▫️msongo mkubwa wa mawazo
kupata wasiwasi kama je watashika tena ujauzito mwingine
▫️kuona aibu na kujihisi wakosaji
▫️kupata mawazo ya kujiua
-Kama ulitoa mimba na unaanza kupata dalili hizi hapa juu, chukua hatua mapema, onana na mtaalamu wa afya ya akili kupata ushauri wa kina.