Ikiwa Zaidi ya watu milioni 17.5 Duniani hufariki kwa sababu ya mshituko wa Moyo, Habari njema ni kwamba zaidi ya 80% ya mshituko wa moyo huweza kuzuilika.
Mambo ya kufanya kuzuia mshituko wa moyo.
1.Kupata usingizi wa kutosha
Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Marekani (CDC) kinasema kuwa na usingizi usiotosha nyakati za usiku kuna uhusiano na shinikizo la damu, kisukari aina ya 2 na unene wa mwili wa kupindukia – jambo ambalo huathiri moyo moja kwa moja.
Inashauriwa kulala angalau saa 7 kwa siku. Hii ni muhimu kwa ajili ya kuwa na kumbukumbu bora, kutulia, na kuwezesha mfumo wa umeng’enyaji na kusafisha kemikali za mwili.
- Kufanya mazoezi ya mwili. Shirika la afya duniani(WHO) linashauri kwamba watu wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 64 “wafanye mazoezi ya sakila kuanzia 150 hadi 300 ya wastani au dakika 75 hadi 150 ya nguvu zaidi” kwa wiki.
Ni muhimu kukumbuka kwamba mazoezi ya mwili, kama vile kukimbia na kuendesha baiskeli, ndio yanayoimarisha misuli na kuongeza pumzi na viwango vya mapigo ya moyo.
- Kudhibiti wasi wasi
Kwanza kabisa, ni lazima tutofautishe mambo tunayoweza kuyafanya na yale ambayo hatuwezi kuyafanya, matatizo tunayoweza kuyatatua na mambo tusiyoweza kuyatatua “, halafu tuelekeze mawazo yetu kwa yale tunayoweza kuyatatua au kuyabadilisha. - Kuacha matumizi ya vilevi, Tumbaku na Kupunguza matumizi ya chumvi nyingi kwenye chakula.
Kuna uhusiano wa moja kwa moja katika ya mshituko wa Moyo na matumizi ya vilevi na tumbaku. Inashauriwa kwa ambao ni watumiaji kuacha kabisa kwa ajili ya kuepuka madhara yatokanayo na vilevi na tumbaku ikiwa ni pamoja na mshituko wa moyo. Watu wanashauriwa pia kuzingatia mlo wenye chumvi kiasi na matunda mengi na mboga za majani ili kudumisha Afya ya mwili - Tambua viashiria na Jenga tabia ya kupima.
Zaidi ya watu 50% wenye mshituko wa moyo huwa hawana Dalili, WATU kujijengea tabia ya kupima mara kwa mara kama Presha, kisukari, wingi wa mafuta inasaidia kujua tatizo mapema na kuanza kulitibia mapema zaidi.
Lakini pia watu wanashauriwa wanapoona Dalili kama maumivu ya kifua yanayosafiri kwenda kwenye bega|mkono|Taya|Shingo, kutokwa na Jasho jingi wakati wa maumivu, kichefuchefu na kizunguzungu.
.
.
.