HUNTER BIDEN AKUTWA NA HATIA YA MASHTAKA MATATU

0:00

9 / 100

Hunter Biden (54), ambaye ni mtoto wa Rais wa Marekani Joe Biden, amekutwa na hatia katika Mashtaka yote matatu ya uhalifu yaliyokuwa yakimkabili.

Jopo la waamuzi 12 wamemkuta Hunter na kosa la kulaghai kuhusu matumizi ya dawa za kulevya wakati alipokuwa akinunua bunduki mwaka 2018.

Makosa mengine ni kutoa taarifa za ulaghai kwa muuzaji wa silaha na kumiliki silaha akiwa ni mraibu wa dawa za kulevya kinyume na sheria.

Hukumu ya kesi hii inaweza kuwa kifungo cha hadi miaka 25, hata hivyo hukumu kubwa na ndefu kiasi hiki hutolewa kwa nadra kwa mkosaji wa mara ya kwanza.

Hunter anakuwa mtoto wa kwanza wa Rais wa Marekani aliye madarakani kukutwa na hatia ya uhalifu.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Msafara wa Kardinali Rugambwa wapata ajali
Don't miss out!
Invalid email address