TEUZI ZA RAIS SAMIA SULUHU HIVI LEO

0

0:00

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali ambapo amemteua Balozi John Simbachawene kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara.

Kabla ya uteuzi huo Balozi Simbachawene alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais Ikulu.

Amemteua Nkoba Mabula kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia utalii ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais Ikulu.

Benedict Wakulyamba ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Maliasili na Utalii anayeshughulikia maliasili.

Rais pia amemteua Dkt. Habib Kambanga kuwa Balozi ambapo Kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais Ikulu.

Wengine walioteuluwa ni Ally Mketo kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe na Jaji Mary Levira kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama akichukua nafasi ya Jaji Gerald Ndika ambaye amemaliza muda wake.

Dkt. Leonard Akwilapo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Dkt. Akwilapo ni Katibu Mkuu Mstaafu na
Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Dodoma.

Rais amemteua Dkt. Noel Mbonde kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala
ya Chuo cha Ufundi Arusha.

Dkt. Mbonde ni Mkurugenzi Mstafu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  3 THINGS YOU NEED TO DO TO AVOID GETTING CAUGHT IN UNHEALTHY RELATIONSHIPS
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading