Ifahamu Eid Al-Adh’haa au Sikukuu Ya Kuchinja

0:00

9 / 100

Ikiwa leo ni siku ya Waumini wa dini ya Kiisalam wakiadhimisha Sikukuu ya Eid Ul Adh’haa au ‘Sikukuu ya kuchinja’

Tuifahamu siku hii maalum ni siku gani hasa!!

Sikukuu hii huashiria kuisha kwa ibada ya Hija eneo la Mina, nchini Saudi Arabia, lakini huadhimishwa na Waislamu duniani kote kama ishara ya kumbukumbu ya imani aliyoionyesha Nabii Ibrahimu (AS).

Eid Al-Adha huanza siku ya kumi ya Dhu’l-Hijja, mwezi wa mwisho kwenye kalenda ya Kiislamu, na hudumu kwa muda wa siku nne. Huanza baada ya siku ambayo Waislamu kumaliza ibada ya Hija wakishuka kutoka katika Mlima wa Arafah.

Sikukuu hii husherehekewa na Waislamu duniani kote, kama zilivyo tamaduni za imani ya dini nyingine.

Lakini Eid Al-Adh’haa ni nini?

Historia ya Eid. Eid Al-Adha, ni sikukuu ya Kiislamu inayoadhimishwa kukumbuka tukio la Nabii Ibrahimu (AS) kuwa tayari kumtoa sadaka mwanaye wa pekee Ismail (AS), kwa kumchinja kama alivyoagizwa na Mwenyezi Mungu . Ingawa alikuwa ni mtu mwema na aliyempenda mwanawe; imani yake na kujitoa kwa Mungu vilikuwa na nguvu zaidi kiasi ambacho angeweza kufanya chochote alichoagizwa.

Kitendo cha utayari wa Nabii Ibrahimu kumtoa sadaka mwanaye wa pekee kwaMungu kilipelekea Mungu kutoruhusu kuchinjwa kwa mtoto yule na badala yake akampatia mwanakondoo kuwa mbadala.

Kitendo cha kuchinja mnyama. Kwa wengi walio nje ya imani ya Kiislamu wamekuwa wakilitafsiri hili tukio tofauti. Kinyume chake, Waislamu huwachinja wanyama wao kwa kutanguliza sala kwanza na kuwachinja kwa jina la Mungu, ambaye amewapa mamlaka juu ya wanyama hao na haki ya kuwala. Hata hivyo, Wailsamu wanapolitaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja, ni kutukumbusha kwamba uhai ni kitu kitakatifu. Kwa hiyo kiuhalisia, hukifanya kitendo hiko kwa kumbariki mnyama na kumshukuru Mungu, pamoja na kutambua utakatifu wa maisha ya mnyama.

See also  Kano Court Orders 10 Million Naira Compensation for Ado Bayero: Ruling Details

Nyama hugawiwa kwa familia, jamaa na maskini. Eid Al-Adha pia hujulikana kama ‘Sikukuu ya Kuchinja.’ Kondoo, ng’ombe, mbuzi, au ngamia ni sadaka kwa jina la Mwenyezi Mungu. Nyama itokanayo na sadaka hugawanywa katika mafungu matatu: theluthi moja kwa ajili ya familia, theluthi nyingine kwa marafiki na majirani, na theluthi inayobakia hugawiwa kwa maskini.

Eid Mubarak.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Erik ten Hag slammed Manchester United as...
The Red Devils suffered a late 1-0 loss at Lerkendal...
Read more
SABABU ASLAY NA MBOSSO KUWA MAADUI ...
MASTORI Aslay ndie chanzo cha beef zito kati yao !!...
Read more
GOD VERSUS DEVIL: Who Will Win Soul...
PROLIFIC NEWS You have many celebrities deleting post on social...
Read more
Profesa RWEKAZA MUKANDALA AFUNGUKA MAZITO YA MV...
HABARI KUU Profesa Rwekaza Mukandala amesema kuzama kwa Mv. Bukoba...
Read more
Ronaldo double helps Portugal reach quarters with...
PORTO, Portugal, 🇵🇹 - Portugal sealed a Nations League quarter-final...
Read more

Leave a Reply