Mpango amwakilisha Rais Samia Kwenye Mazishi ya Saulos Chilima

0:00

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Kitaifa ya Makamu wa Rais wa Malawi Dkt. Saulos Chilima aliyefariki dunia katika ajali ya ndege.

Ibada ya mazishi hayo imefanyika katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi.

Akitoa salamu za rambirambi Dkt. mpango amesema Tanzania inatoa pole na kuungana na waombolezaji wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki kigumu.

Amesema Hayati Chilima alikuwa kiongozi imara, mwanamajumui wa kweli wa Afrika ambaye wakati wote alitanguliza mbele maslahi ya wananchi anaowaongoza na Afrika kwa ujumla.

Pia amemtaja Hayati Chilima kama kiongozi aliyesimamia umoja, amani na usalama, mageuzi ya kiuchumi ya Malawi na utawala wa kidemokrasia nchini Malawi.

Makamu wa Rais amesema wananchi wa Malawi na Ukanda wote kwa ujumla wanapaswa kumuenzi Hayati Chilima kwa kuendeleza yale aliyosimamia na kuendelea kumuombea apumzike kwa amani.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Council of Legal Education Acknowledges Exam Result...
The Council of Legal Education has acknowledged a mix-up in...
Read more
Odinga Denies Bribery Allegations, Reaffirms Solidarity with...
Azimio la Umoja - One Kenya Coalition principal Raila Odinga...
Read more
MWALIMU MAGANGA AFUTWA KAZI ...
HABARI KUU. Tume ya utumishi ya Walimu Tanzania (TSC) imemsimamisha...
Read more
SABABU YA KIFO CHA GADNER HABASH MTANGAZAJI...
NYOTA WETU Mtangazaji maarufu wa kituo cha radio cha...
Read more
MWILI WA MKUU WA MAJESHI KENYA KUZIKWA...
HABARI KUU Mwili wa Mkuu wa Majeshi Nchini Kenya, (CDF)...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  The National Assembly to Debate Inspector-General Nominee Report

Leave a Reply