MAKALA
Luhaga Mpina ameeleza umma, maamuzi ya mawaziri, Hussein Bashe (Kilimo) na Mwigulu Nchemba (Fedha) yamepoteza mapato ya Serikali zaidi ya Sh580 bilioni.
Kwa mantiki ndogo, upotevu wa fedha za Serikali ni zaidi ya ufisadi wa RICHMOND ambao ulimfanya Waziri Mkuu, Edward Lowassa kuwajibika kwa kujiuzulu.
Badala ya bunge kuunda kamati teule kuchunguza taarifa kwa kuwa upo ushahidi wa nyaraka, bunge la CCM limemuita Luhaga Mpina kamati ya maadili.
Luhaga Mpina amepelekwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kilichoitwa kuingilia madaraka ya Spika kwa kuwasilisha ushahidi wa tuhuma kwa umma.
Bunge la CCM limechoka. Tuhuma hizo zimebebwa na ushahidi. Bunge lilitakiwa kuunda kamati teule ya bunge, siyo kumpeleka kamati ya maadili ya bunge
Upotevu wa mapato ya serikali Sh580 bilioni ni zaidi ya ufisadi mkubwa wowote uliowahi kutikisa serikali na bunge ukiondoa upotevu wa TZS trilioni 1 enzi za JPM.
Tegeta ESCROW (Sh306bn), EPA (TZS 133bn), Mwananchi Gold (Sh272bn), Meremeta (Sh155bn), Mfuko wa kuwezesha uagizaji – CIS (Sh200 bilioni).
Ufisadi wote, mmoja mmoja haujafika katika ufisadi (Sh580bn) ambao unatajwa na Luhaga Mpina kuwa ulisababishwa na Hussein Bashe na Mwigulu Nchemba.
Baraza la usalama la Taifa (2014) lilikutana na kupitia taarifa ya uchunguzi PCCB kuhusu ufisadi wa ESCROW (Sh306bn) kwanini ufisadi wa Sh580bn upuuzwe?
PCCB walifanya uchunguzi ufisadi wa ESCROW na kukabidhi taarifa kwa Rais Jakaya Kikwete, kwanini uchunguzi wa Sh580 bilioni usifanyike? Analindwa nani?
Uchunguzi wa PCCB ulionesha taarifa ya Mkombozi Bank (20/01/14-14/08/14) na malipo kutoka akaunti ya VIP engineering kwenda kwa watu mbalimbali.
Tunashangaa, badala ya bunge kuunda kamati teule kuchunguza taarifa na kuujuza umma, bunge limeamua kumtisha Mpina kwa kutoa ushahidi kwa umma.
Hizo ni juhudi za kumnyamazisha Luhaga Mpina na kuwatetea watu hao anaowatuhumu kwa ufisadi na upotevu wa fedha za serikali zaidi ya Sh580 bilioni.