0:00
HABARI KUU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Hassan Babu kufuatia kifo cha aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Tixon Nzunda kufuatia ajali ya gari.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, ajali hiyo iliyochukua maisha ya Dkt Nzunda na dereva wake ilitokea majira ya saa nane mchana katika eneo la njiapanda ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro alipokuwa kwenye ziara ya kikazi.
Rais Samia anawapa pole ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu. Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi.
Related Posts 📫
HARUFU MBAYA UKENI:
Kutokwa na harufu mbaya ukeni ni tatizo linalowasumbua...
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambaye pia ni...
Michezo
Chama cha soka England (FA) kinatazamia kumpa kandarasi Mkufunzi wa...
HABARI KUU
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika...