SIASA ZA SUKARI NA SUKARI YA SIASA

0

0:00

13 / 100

MAKALA

Dr. Benson Bagonza

SIASA ZA SUKARI Vs SUKARI YA SIASA

Sukari ni tamu lakini inalimwa mahali pagumu. Siku za karibuni imekuwa ghali sana. Huku vijijini familia inanunua kilo moja na kuitunza kwa ajili ya mgonjwa atakayeugua maralia.

Liko tabaka ambalo utamu wa sukari ni sumu kwao. Kwao hawa, sukari ikipanda si tatizo. Lakini ziko bidhaa nyingi sana zinazohitaji sukari. Kwa hiyo hitaji la sukari ni kubwa. Hali hii huzalisha SIASA ZA SUKARI yaani:

  1. Kutengeneza uhaba ili kuinua hitaji.
  2. Kutengeneza urasimu wa kuziba
    pengo la uhitaji wa sukari.
  3. Kutengeneza mgogoro kati ya
    wazalishaji, walaji, na waagizaji wa
    nje.

Haya matatu yakitengemaa, kinachofuata ni SUKARI YA SIASA, yaani:

-Kununuana kikweli kweli ili kuwezesha ama vibali vya uagizaji au upandishaji wa bei ya sukari inayozalishwa ndani.

-Kusingiziana na kuzushiana ikiwa kununuana kumeshindikana.

-Matumizi mabaya ya mamlaka ya uteuzi, bunge, na vyombo vya habari.

MATOKEO YAKE:

a) Katika minyukano yote hii, mlaji maskini anasahaulika na hana mtetezi. Bei ya sukari katika mipaka yote (Mtukula, Sirari, Tunduma, Kabanga) iko chini kuliko sukari tunayozalisha. Tumbo halina uzalendo. Bei inaamua mgogoro tumboni na ndiyo maana polisi na vizuizi haviishi mipakani. Rais ondoa vizuizi, mgogoro wa sukari utaisha wenyewe.

b) Viwanda vya sukari vinapata misamaha mbalimbali, ardhi, ujira mdogo kwa vibarua nk. Na bado bei ya sukari inakuwa kubwa. Hata mikoa iliyo karibu na viwanda haina unafuu wowote. Kuna mzimu gani hapa?

c) Sukari inalichafua bunge letu lilikosa mwekezaji. Kutwa kucha kutuhumiana. Hatuoni maslahi ya mlaji wa kawaida wa sukari.

See also  Egypt, Senegal, Uganda and DR Congo seal African Nations Cup finals places

d) Upofu mkubwa umewapata watawala wetu. Badala ya kushughulika na uwongo/ukweli wa wanaotuhumiana, wanashughulika na NJIA za kutuhumiana. Katika mchakato huo, mwathirika mkuu ni Mlaji wa sukari na ndugu yetu Ukweli.

e) Kwangu mimi, BUNGE ni mahali patakatifu kuliko Ikulu na Mahakamani.
Lakini hivi sasa panatisha. Kutokana na “sukari ya siasa” ni vigumu kumjua mkweli na mwongo. Heshima ya Kiti na viapo vinagwaya mbele ya sukari ya siasa. Kwetu sisi walaji wa sukari, mkweli ni anayetetea bei ishuke ili tunywe sukari na kupata kisukari wakati hatuna bima.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Please disable your adblocker or whitelist this site!

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading