MAWAKILI KUMBURUZA MAHAKAMANI MKUU WA WILAYA KWA UDHALILISHAJI WANAWAKE

0:00

9 / 100

HABARI KUU

Wakili wa kujitegema nchini Wakili Peter Madeleka amesema wanajiandaa kufungua shauri la fidia ya shilingi za Kitanzania bilioni 36 dhidi ya mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar es salam Hassan Bomboko kwa udhalilishaji wa watu 36 alioagiza wamakatwe akiwatuhumu kujihusisha na biashara ya ngono na kisha kuachiliwa huru.

Wakili Madeleka ametoa kauli hiyo akizungumza na Watetezi tv na kuongeza kuwa hadi sasa watu hao ambao ni Wanawake na wanaume hawajasomewa mashtaka licha ya jana 19 June 2024 kupelekwa mahakamani .

Amesema tayari wameshajiandaa kwa ajili ya shauri hilo kwa lengo la kudai haki za watuhumiwa hao ambao amedai wanakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu ikiwemo kunyimwa taulo za kike kwa wanawake ambao wapo katika siku zao.

Mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar es salam Hassan Bomboko mwishoni mwa wiki iliyopita aliendesha Oparesheni ya kukamata wanaojihusisha na Biashara ya ngono katika wilaya hiyo.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Waliomuua Mtoto Asimwe Wafikishwa Mahakamani
HABARI KUU Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye UalbinoAsimwe Novath...
Read more
TIPS TO PREVENT RESPIRATORY INFECTIONS IN POULTRY
In my visit to poultry farms a day won't pass...
Read more
Spain ease to 3-0 win over Serbia...
CORDOBA, Spain, 🇪🇸 - European champions Spain claimed a place...
Read more
JINSI SERIKALI YA TANZANIA INAVYOTUMIA MABILIONI KWAAJILI...
MAKALA Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas...
Read more
HOW TO BE ALWAYS HAPPY IN LIFE
Always remember that there is nobody on this earth that...
Read more
See also  Nigerian influencer Aproko Doctor opens up about his recovery journey after undergoing surgery for a brain tumor.

Leave a Reply